Pata taarifa kuu
KENYA-UCHUMI-MAZINGIRA

Wanamazingira wapinga mradi wa serikali wa kuzalisha kawi ya mkaa wa mawe Kenya

Wakati ulimwengu ukielekea katika mpango wa kawi safi kwa kupunguza uharibifu wa mazingira, nchini Kenya wadau wamepinga mradi wa serikali wa kuzalisha kawi ya mkaa wa mawe wakisema madhara yake kwa mazingira ni makubwa mno.

Wakaazi wengi eneo la Lamu wamepinga mradi wa serikali wa kuzalisha kawi ya mkaa wa mawe Kenya
Wakaazi wengi eneo la Lamu wamepinga mradi wa serikali wa kuzalisha kawi ya mkaa wa mawe Kenya Erik Hersman/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Mradi huo wa ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha kawi kupitia mkaa wa mawe unatarajiwa kuzalisha megawati 1,050japo wanamazingira wanahoji uhalali wake kwa mazingira.

“Coal inapatikana sehemu za bahari, samaki watapotea pale Mwanzo kunaanza kufa mimea pale, kisha madhara ya ngozi, madhara ni mengi hata kuliko faida, “ amesema Hamisa Zaja, katibu wa shirika la mazingira la United green movement.

Mwekezaji na mtafiti wa uchumi Abdala Fadhili, anasema iwapo serikali iteandelea na mradi huo wa kawi ya mkaa wa mawe, eneo hilo la Lamu litaathirika pakubwa kimazingira.

“Watalii muhimu hawaji tena Lamu, upande wa kilimo hatutauza mazao yetu, samaki, inasemekana kutakuwa na chembechembe za mercury, mercury nisumu” amesema Abdala Fadhili.

Mataifa ulimwenguni yamekuwa yakiangazia sana uzalishaji wa kawi safi, hali ambayo wananchi wengi eneo hilo la Lamu wamepinga mradi huo.

Upande wa serikali kupitia msemaji wake Cyrus Oguna, inasema teknolojia itakayotumika katika kiwanda hicho haitakuwa na madhara.

“Teknolojia tunayotumia ni bora zaidi ulimwenguni, ni teknolojia ambayo haijawahitumika Afrika, na hivyo Kenya itakuwa ya kwanza kutumia teknolojia hiyo” , amesema Cyrus Oguna, msemaji wa serikali ya Kenya.

Kiwanda hicho kinatarajiwa kuwa cha kwanza na cha kipekee nchini kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.