Pata taarifa kuu
KENYA-SENSA-MAENDELEO-SIASA

Matokeo ya sensa : Idadi ya wakenya yafikia Milioni 47.5

Idadi ya Wakenya imeongezeka na kufikia Milioni 47,564,296, kwa mujibu wa Tume ya taifa ya takwimu, baada ya zoezi la sensa, kufanyika nchini humo mwezi Agosti.

Sensa ya Kenya ilifanyika mwezi Agosti.
Sensa ya Kenya ilifanyika mwezi Agosti. KNBS
Matangazo ya kibiashara

Sensa hufanyika kila baada ya miaka 10 nchini Kenya, kuna ongezeko la watu Milioni tisa, kwa kipindi hicho.

Takwimu zinaonesha kuwa, kuna Wanawake Milioni 24 huu wanaume wakiwa Milioni 23.6 huku watu wenye jinsia tata wakiwa 1,524.

Rais Uhuru Kenyatta amepokea ripoti ya zoezi hilo la sensa, na kusema Kenya imekuwa nchi ya kwanza duniani, kupata matokeo ya idadi ya watu wanaoishi nchini humo kwa kipindi kifupiti cha miezi miwili.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kaunti ya Nairobi inaongoza kwa wingi wa watu, ambao wamekadiriwa kuwa zaidi ya Milioni 4, ikifuatwa na Kiambu, Nakuru, Kakamega na Kilifi.

Haya ni matokeo ya kwanza ya Sensa nchini humo, baada ya nchi hiyo kupata Katiba mpya mwaka 2010 na idadi hiyo inatarajiwa kuisaidia serikali kuweka mipangilio ya maendeleo na kugawa rasilimali mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya raia wake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.