Pata taarifa kuu
TANZANIA-BURUNDI-MAWASILIANO

Tanzania yatoa huduma za mtandao wa intarnet kwa Burundi

Kampuni ya mawasiliano nchini Tanzania TTCL imesaini mkataba na kampuni ya Burundi BBS,kuunganisha mtandao wa Internet katika nchi hiyo jirani.

Shughuli za kibiashara pia zinatarajiwa kuimarishwa kati nchi hizi mbili, kutokana na Burundi kuwa na mtandao imara.
Shughuli za kibiashara pia zinatarajiwa kuimarishwa kati nchi hizi mbili, kutokana na Burundi kuwa na mtandao imara. ©Facebook
Matangazo ya kibiashara

Mradi huo utaigharimu serikali ya Burundi Dola Milioni 6, na kwa mujibu wa mkataba huo, utatekelezwa kwa kipindi cha miaka 10.

Mkurugenzi wa TTCL Waziri Kindamba amewahakikishia wananchi wa Burundi kuwa kampuni hiyo itahakikisha kuwa inapata mtandao bora wa Internet.

Aidha, amesema kuwa mkataba huo utasaidia TTCL kupanua huduma zake za kutoa Internet katika mataifa mengine ya Afrika Mashariki na Kusini mwa bara la Afrika.

Shughuli za kibiashara pia zinatarajiwa kuimarishwa kati nchi hizi mbili, kutokana na Burundi kuwa na mtandao imara.

Kampuni nyingine ya mawasiliano nchini Tanzania Halotel, iliyokuwa inatarajiwa pia kutoa huduma hiyo, haikushirikishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.