Pata taarifa kuu
RWANDA-UNHCR-LIBYA-UN-AU

Kundi la kwanza la wakimbizi kutoka Libya wawasili nchini Rwanda

Kundi la kwanza la wakimbizi 66 wakiwemo watoto, akina mama na watu wanaohitaji msaada wa haraka, ambao wamekuwa wakizuiwa nchini Libya, wamewasili jijini Kigali nchini Rwanda, na kupelekwa katika kambi iliyoandaliwa kwa ajili yao, Mashariki mwa nchi hiyo.

Wakimbizi kutoka barani Afrika wakiwasili katika uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Kigali,  Septemba 26 2019
Wakimbizi kutoka barani Afrika wakiwasili katika uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Kigali, Septemba 26 2019 www.newtimes.co.rw
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa wakimbizi waliowasili Alhamisi usiku, ni mtoto mwenye umri wa miezi miwili, aliyezaliwa na wazazi kutoka Somalia, lakini walijikuta wakiwa wamekwama nchini Libya.

Awamu ya pili ya wakimbizi wapatao 125, wanatarajiwa kuwasili katika tarehe 10-12 mwezi Oktoba kwa mujibu wa afisa wa juu wa Umoja wa Mataifa.

"Tumetua" Huu ndio ujumbe ulioandikwa katika ukurasa wa Twitter wa Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi.

Mapema mwezi huu, Rwanda ilitia saini mkataba na Umoja wa Afrika na Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wkaimbizi UNHCR, kwa nchi hiyo kuwakarabisha wakimbizi kutoka mataifa ya Afrika waliokwama nchini Libya wakiwa mbioni kwenda barani Ulaya.

Serikali ya Rwanda imesema iko tayari kuwapa hifadhi wakimbizi 30,000 kati ya 42,000 wanaozuiwa nchini Libya lakini itawakaribisha kwa utaratibu maalum  wa kuwakubali 500 kwa hatua kadhaa, ili kuzuia nchi hiyo yenye watu Milioni 12 isiwe na mzigo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.