Pata taarifa kuu
BURUNDI-SOMALIA-AMISOM-USALAMA

Wanajeshi kadhaa wa Burundi wauawa katika shambulio Somalia

Askari zaidi 12 wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika (AMISOM) kutoka Burundi wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la kuvizia nchini Somalia.

Askari wa kikosi cha Amisom kutoka Burundi wakipiga doria (picha ya kumbukumbu).
Askari wa kikosi cha Amisom kutoka Burundi wakipiga doria (picha ya kumbukumbu). Reuters/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Shumbulio hilo lilitokea Jumamosi Septemba 14 na liliendeshwa na wanamgambo wa Kiislamu wa kundi la Al Shabab lenye mafungamano na al-Qaeda nchini Somalia.

Msafara wao ulishambuliwa wakati ulipokuwa ukirudi kwenye kambi yao kwenye barabara muhimu inayounganisha mji mkuu Mogadishu na Jimbo la Shabelle. Kikosi hicho cha jeshi la Amisom kilikuwa kinarudi kutoka Mogadishu.

kikisi hicho kama kawaida yake kilikuwa kinasindikiza malori yaliyokuwa yanasafrisha chakula kutoka Jowhar, mji mkubwa, unaopatikana kilomita 90 kaskazini magharibi mwa Somalia kwenda kwenye masoko ya mji mkuu Mogadishu.

Karibu na kijiji cha Balcad, katikati ya miji hiyo miwili, msafara huo wa kikosi cha AMISOM ulishambuliwa na wanamgambo wa Al Shabab. Kwa mujibu wa mashahidi, mapigano hayo mabaya yalidumu kama dakika ishirini.

Barabara hiyo, na kijiji hicho cha Balcad, vinajulikana kuwa hatari. Jana asubihi, maafisa wawili wa serikali za mitaa na dereva wao waliuawa baada ya gari yao kukanyaga kifaa cha kulipuka karibu na eneo la shambulio lililotokea Jumamosi.

Mwezi Machi 2018, wanajeshi watano wa Burundi waliuawa sehemu hiyo katika shambulio kama hilo lililotekelezwa na kundi la wanamgambo wa Al Shabab.

Licha ya juhudi za AMISOM, vita kwa jaili ya kulinda barabara hiyo haijazaa matunda. Bara bara hiyo ni muhimu kwa mamlaka ya Somalia kwani inaunganisha mkoa wa kilimo wa mji mkubwa wa Jowhar na Mogadishu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.