Pata taarifa kuu
UGANDA-BOBI-SIASA-USALAMA

Bobi Wine: Tutaendelea kutetea haki ya wanyonge

Mahakama nchini Uganda imemfungulia mashtaka mbunge wa upinzani na mwanamuzi Muziki Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine na watu wengine zaidi ya 20 kwa kumkasirisha rais Yoweri Museveni.

Mwanamuziki Bobi Wine ni mpinzani mkuu wa Rais Museweni nchini Uganda (hapa alikuwa mbele ya mahakama ya Kampala mwezi Aprili 2019).
Mwanamuziki Bobi Wine ni mpinzani mkuu wa Rais Museweni nchini Uganda (hapa alikuwa mbele ya mahakama ya Kampala mwezi Aprili 2019). Nicholas BAMULANZEKI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mbunge huyo aliyetangaza nia ya kuwania urais mwaka 2021, aliongezewa shtaka hilo, baada ya kuanza kwa kesi hiyo Jumanne wiki hii jijini Kampala, kutokana na mashatka mengine yanayomkabili ya kurushia mawe msafara wa rais Museveni mwaka uliopita.

“Mashtaka mengi ya kipumbavu yanaendelea kuwasilishwa dhidi yetu, napenda kuiambia dunia kuwa, hii haitutishi kwa njia yoyote ile”, amesema Bobi Wine.

Wine nakabiliwa na kifungo cha maisha jela, iwapo atapatikana na hatia.

Wine ambaye jina lake ni Robert Kyagulani bado anakabiliwa na mashtaka katika mahakama nyengine kwa kuongoza maandamano dhidi ya sheria inayoweka kodi katika mitandao ya kijamii pamoja na biashara zinazofanywa kupitia malipo ya simu za rununu 2018.

Msanii huyo ambaye amekuwa mwanasiasa wa upinzani anayepinga utawala wa miongo mitatau ya rais Museveni hivi majuzi alitangaza kwamba atawania urais katika uchaguzi wa 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.