Pata taarifa kuu
KENYA-MAREKANI-USALAMA-UGAIDI

Marekani: Raia wetu mmoja ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulio Kenya

Raia mmoja wa Marekani ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulio linaloendelea dhidi ya hoteli ya kifahari ya DusitD2 jijini Nairobi, nchini Kenya, afisa mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema.

Watu waendelea kuokolewa kutoka Hoteli ya Dusit, kifahari ya DusitD2, Nairobi, Kenya, Januari 15, 2019.
Watu waendelea kuokolewa kutoka Hoteli ya Dusit, kifahari ya DusitD2, Nairobi, Kenya, Januari 15, 2019. REUTERS / Njeri Mwangi
Matangazo ya kibiashara

"Tunaweza kuthibitisha kwamba raia mmoja wa Marekani ameuawa katika shambulio hilo na tunatuma rambi rambi zetu kwa familia na marafiki," afisa huyo amesema.

Afisa huyo ambaye hakitaja jina lake, amekataa kutoa maelezo zaidi.

Watu 15 ndio wanasadikiwa kuwa wameuawa katika shambulio hilo kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya polisi nchini Kenya.

Mashahidi wanasema mmmoja wa washambuliaji ni miongoni mwa watu waliouawa.

Kundi la wanamgambo kutoka Somalia la Al Shabab, lenye mafungamano na Al Qaeda, limekiri kuhusika na shambulio hilo.

"Marekani inalaani vikali shambulio hilo la kutisha dhidi ya hoteli ya kifahari ya DusitD2 jijini Nairobi," amesema Bob Godec, balozi wa Marekani nchini Kenya."

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat amelaani vikali shambulio la Hoteli ya kifahari ya DusitD2 jijini Nairobi.

Katika taarifa yake, Faki amevisifu vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwa kuchukua hatua za uokozi wa raia na kupambana na wahalifu mapema iwezekanavyo.

Kenya ilianza kushuhudia milipuko ya kigaidi kutoka kwa kundi la Al Shabab mwaka 2011, baada ya kuwatuma wanajeshi wake nchini Somalia, kupambana na kundi hilo la kigaidi ambalo linapambana na serikali ya Mogadishu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.