Pata taarifa kuu
BURUNDI-AU-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

AU yajaribu kuishawishi Burundi kushiriki mazungumzo mapya

Ujumbe wa umoja wa Afrika unaoongozwa na Smail Chergui uko nchini Burundi kwa siku tatu sasa kujaribu kushawishi upande wa Serikali ukubali kuwepo kwa mazungumzo mapya siku za usoni.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Juni 7,  2018.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Juni 7, 2018. REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya amani ya Burundi yaliyokuwa yanasimamiwa na rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa yalimalizika hivi karibuni katika kikao chake cha tano na cha mwisho bila kuzaa matunda yoyote.

Wadadisi wanasema baada ya mazungumzo hayo kumalizika bila kuzaa matunda yoyote, kuna uwezekano Umoja wa Afrika kushughulikia mgogoro unaoikabili nchi ya Burundi.

Ni swali ambalo wengi wangelipenda kufahamu baada ya kushindwa kupatikana kwa suluhu ya mgogoro wa Burundi hasa kutokana na serikali pamoja na washirika wake kususia vikao hivyo.

Muwezeshaji katika mgogoro huo Benjamin William Mkapa sasa anarudisha jukumu kwa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki waliomteuwa ambao hata hivyo wanatuhumiwa kutompa ushirikiano wa kutosha.

Baada ya kuongoza usuluhishi kwa kipindi cha miaka 3 kilichoanza mwaka 2015 baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa 3, miezi kadhaa baadae Benjamin Mkapa aliepewa jukumu la kuratibu mazungumzo na ambapo hivi karibuni ndipo alitangaza kufikia tamati ya jukumu lake.

Hayo yanajiri wakati ujumbe wa halamashauri ya amani na usalama kwenye shirika la Umoja wa Afrika ukiongozwa na Smaïl Chergui uko ziarani nchini Burundi tangu mwanzoni mwa wiki hii kwa wajili ya mashauriano na viongozi wa nchi hiyo.

Ujumbe huo tayari umeshakuwa na mazungumzo na maafisa kadhaa wa serikali ya Bujumbura ikiwa ni pamoja na Makamu wa kwanza wa rais Gaston Sindimwo, waziri wa Burundi wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa kimataifa, yule wa Ulinzi pamoja pia na yule wa Mambo ya Ndani.

Imedaiwa kuwa ziara hii ya Bw Chergui inalenga kupendekeza kwa viongozi wa Burundi utayarifu wa Umoja wa Afrika kuishindikiza Burundi katika mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2020 ili uwe uchaguzi wa haki tena wa kweli.

 Badala yake Umoja wa Afrika umejikubalisha kuitetea Burundi kwenye Umoja wa Ulaya ili iondolewe vikwazo ilivyowekewa na umoja huo wa ulaya na ambavyo vimekuwa na athari nyingi kwenye uchumi wa nchi hiyo.

 Hata hivyo Smail Chergui hadi sasa hajafanikiwa kukutana na rais wa Burundi Pierre NKURUNZIZA ambaye kwa muda mrefu anakuwa katika kijiji chake cha asili kaskazini mwa nchi hiyo, mkoani Ngozi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.