Pata taarifa kuu
KENYA-MAUAJI-MWANAHABARI-MAHAKAMA

Mwanahabari na mchumba wake waendelea kuzuiwa kwa madai ya mauaji

Mahakama Kuu jijini Nairobi nchini Kenya imeagiza kuendelea kuzuiwa kwa washukiwa wawili wa mauaji ya mwanadada Monica Kimani, aliyepatikana ameuawa nyumbani kwake mwezi Septemba.

Jacque Maribe (Kushoto) akiwa na mpenzi wake Joseph Irungu (Kulia) washukiwa wa mauaji ya mwanadada Monica Kimani, wakiwa Mahakamani Oktoba 09 2018 jijini Nairobi
Jacque Maribe (Kushoto) akiwa na mpenzi wake Joseph Irungu (Kulia) washukiwa wa mauaji ya mwanadada Monica Kimani, wakiwa Mahakamani Oktoba 09 2018 jijini Nairobi NationBreaking
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Mashtaka, wamesema watamfungulia kesi ya mauaji Mwanabahari maarufu nchini humo Jacque Maribe na mpenzi wake Joseph Irungu ambaye ndio mshukiwa mkuu.

Jaji Jessi Lessit amesema wawili hao watazuiwa hadi siku ya Jumatatu wiki ijayo, na kuagiza kuwa Bi. Maribe afanyiwe uchunguzi wa kiakili katika Hospitali ya wagonjwa wa akili kabla ya kujibu mashtaka yanayomkabili.

Irungu naye ametakiwa kupewa huduma ya matibabu baada ya kupata jeraha la bega. Hata hivyo, viongozi wa mashtaka wanadai kuwa mshukiwa huyo alijipiga risasi mwenyewe wala hakushambuliwa.

Kiongozi wa Mashtaka Noordin Haji, ameagiza wawili hao kufunguliwa kesi ya mauaji kwa madai kuwa walishirikiana kumuua mwanadada huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.