Upinzani ulio uhamishoni kushiriki mazungumzo ya amani ya Burundi Arusha
Wanasiasa wa Burundi waishio uhamishoni wamesema watakuwa tayari kushiriki katika mazungumzo ya kusaka suluhus ya mzozo wa Burundi yalioitishwa na mratibu wa mazungumzo hayo rais wa zamani wa Tanzania Benjamin William Mkapa kuanzia Oktoba 18 hadi Oktoba 24 mjini Arusha nchini Tanzania.
Imechapishwa:
Muungano wa wanasiasa waishio uhamishoni Cnared unasema utakuwa tayari kushiriki kwenye mazungumzo hayo ambayo hata hivyo yanakosolewa vikali na baadhi ya mashirika ya kiraia ambayo yanasema hayajaona utashi wowote kutoka kwa serikali ya rais Pierre Nkurunziza kutaka kumaliza mzozo wa kisiasa uliopo.
Onesime Nduwimana msemaji wa muungano wa vyama vya upinzani (Cnared) anaona itakuwa ni fursa nzuri kuona mazungumzo hayo yanawashirikisha wadau wote katika mgogoro wa Burundi, vinginevyo itakuwa ni kupoteza muda na kwamba Warundi wana matarajio makubwa kutoka kwa wadau wote wa kisiasa.
Au terme de la session de consultat° entre le #CNARED et l'équipe de la Facilitation de @WMkapa, l'opposition extérieure dans son ensemble s'est engagée à répondre présente aux négociations à venir et demande au pouvoir de @pnkurunziza de faire de même pr mettre fin à cette crise pic.twitter.com/G4WF0T4GQi
CNARED Burundi (@cnaredburundi) September 8, 2018
Mashirika kadhaa ya kiraia yanaona kuwa mzungumzo hayo yajayo hayatakuwa suluhu ya mzozo uliopo ukizingatia kuwa serikali ya Burundi bado hainaonyesha umuhimu wa kuzungumza na wapinzani wake.
Serikali ya Burundi imekuwa ikipinga kuketi kwenye meza ya mazungumzo na wanasiasa hao kutoka Cnared ikiwashtumu kwamba baadhi yao walihusika katika jaribio la mapinduzi lililotibuliwa Mei 15, 2015.
Machafuko nchini Burundi yamesababisha zaidi ya watu 2000 kuawa kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadamu nchini Burundi na maefu kadhaa kutoroka makazi yao na kukimbilia katika nchi jirani.