Pata taarifa kuu
TANZANIA-MALIASILI-USALAMA

Tanzania yawafunga Tembo kifaa Maalum kukabiliana na Ujangili

Serikali ya nchi ya Tanzania inaendelea na mpango wa kuwafunga vifaa maalum tembo katika hifadhi zake ili kufuatilia mienendo yao ili kukabiliana na tishio la kutoweka kwa Tembo katika Hifadhi za wanyama pori nchini humo kutokana na Ujangili

Tembo akiwa Mbugani
Tembo akiwa Mbugani WWF/Mumbi
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hilo limefadhiliwa na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Shirika la uhifadhi mazingira duniani(WWF) pamoja na Fredkin Concervation fund, Meneja mawasiliano wa Shirika hilo Clarence Msafiri ni Meneja wa Mawasiliano wa shirika hilo alisema wametoa helikopta ili kuiwezesha seriaki ya Tanzania kufanikisha kuwafunga tembo hao katika hifadhi ya Mikumi.

Akizungumzia umuhimu wa zoezi hilo, Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Mikumi iliyopo Morogoro nchini humo Godwell Ole Meing’ataki amesema tembo jike kiongozi ndio huongoza msafara wa tembo katika familia yake kumfunga kifaa hicho kutasaidia kujua idadi yao na kuepuka migogoro iliyokuwa inasababishwa na kutofahamu mienendo yao na hivyo kuingia katika makazi wa wananchi.

Kwa upande wake Mtafiti Mkuu kutoka Taasisi ya taifa ya Utafiti wa Wanayama pori TAWIRI Dakta Edward Kohi alisema mchakato wa kumfunga tembo kifaa hicho maalum huanza kwa kumtafuta tembo jike angani ,baadae daktari wa wanyama pori anamchoma sindano ya usingizi ndio helikopta hushuka taratibu na kumfunga na hatiamae kumwamsha na kuondoka haraka eneo hilo

Akizungumzia mkakati wa serikali ya Tanzania, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya wanyamapori,Wizara ya Malia asili na Utalii Silvanus Atete Okudo anasema ujangili umeathiri kwa kiasi kikubwa idadi ya tembo sasa mpango huo utasaidia kuwahifadhi ambapo mpaka sasa tembo waliopo wanakadiriwa kufikia elfu hamsini tu

Kifaa hicho Kinagharimu kati ya Dola 2000 na 3500.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.