Pata taarifa kuu
BURUNDI-KATIBA-SIASA-USALAMA

Warundi waendelea kusubiri matokeo ya kura ya maoni

Warundi walijitokeza kuipigia kura marekebisho ya Katiba Alhamisi wiki hii (Mei 17) ambayo kwa hali yoyote itamruhusu Rais Pierre Nkurunziza kusalia madarakani akiwa na mamlaka kamili hadi mwaka 2034.

Mwanamke akipiga kura katika kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba, Ciri kaskazini mwa Burundi. Mei 17, 2018.
Mwanamke akipiga kura katika kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba, Ciri kaskazini mwa Burundi. Mei 17, 2018. STR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi kwa jumla ulifanyika kwa utulivu na uliitikiwa na watu wengi, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi (CENI) na mashahidi. Hakuna anayejua wakati ambapo matokeo yatatangazwa, lakini kura hiyo iligubikwa na kasoro mbalimbali. Burundi ilitumbukia katika mgogoro mkubwa wa kisiasa kutokana na hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Vituo vya kupigia kura vilifungwa saa 10 alaasiri (saa za Afrika ya Kati) kama ilivyoamuliwa na Tume ya Uchaguzi nchini humo (CENI). Katika baadhi ya vituo vya kupigia kura kiwango cha ushiriki kilifikia karibu 70%, kwa mujibu wa tovuti inayoegemea upande wa serikali. Lakini CENI haikutaka kutoa kiwango cha ushiriki kwa siku nzima ya jana.

Vijana wa chama tawala, Imbonerakure, ambao Umoja wa Mataifa, unawaita kuwa ni wanamgambo, walikua wakiwafanyia vitisho raia na kuwataka waende kupiga kura ya Ndiyo "Ego" kwa lugha ya Kirundi.

Chama kilichokuwa na nguvu kilikuwa kikiita kura ya asubuhi, lakini si kila mtu aliyekuja kwa moyo mzuri. Utawala na Imbonerakure, vijana wa chama cha tawala ambacho Umoja wa Mataifa huwaita wanamgambo, wametoka nyumba kwa nyumba wakihimiza wale wanaokataa kupigia kura.

Zoezi la kuhesabu kura lilianza baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa. Lakini haijajulikana wakati matokeo yatatangazwa.

Mashirika yasiyo ya kiserikali kwa miezi kadhaa yameshutumu utawala kuanzisha kampeni ya kuwatia uoga Warundi na kuwalazimisha kupiga kura ya Ndiyo "Ego". Hata hivyo, muungano wa Amizero y' Abarundi wa Agathon Rwasa umesema kuwa kura hiyo iligibikwa na wizi na udanganyifu mkubwa, huku ukibaini kwamba maafisa wake walifukuzwa katiika vituo vya kupigia kura na wengine walikamatwa na hawajulikani walik. Muungano huo unasema kuwa wapiga kura walilazimishwa kupiga kura yaa Ndiyo, lakini chama tawala, CNDD-FDD, kimefutilia mbali shutma hizo.

Kura ya Hapana "Oya" ilishinda, ni wazi, inaonekana, hata katika hali hii ngumu ambapo, wapiga kura wamekua wakifanyiwa vitisho wengine kukamatwa. Utawala huu wa kiimla, na Katiba hii inayotenga baadhi ya watu, siku moja utaanguka, muungano wa Amizero y'Abarundi umesema katika taarifa yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.