Pata taarifa kuu
KENYA-UTAFITI-UCHUMI

Satelaiti iliyotengenezwa Kenya kurushwa anga za juu Ijumaa hii

Kenya imetengeneza Satelaiti yake ya kwanza kabisa ambayo imepangiwa kurushwa anga za juu leo Ijumaa. Kwenye satelaiti hiyo zimebandikwa kamera mbili pamoja na vyombo vya kunasa na kupeperusha sauti.

Mawasiliano halisi ya kimataifa ya kiasi kikubwa yanayowezeshwa na satellite ya Micius.
Mawasiliano halisi ya kimataifa ya kiasi kikubwa yanayowezeshwa na satellite ya Micius. Phys.org
Matangazo ya kibiashara

Uzinduzi wa satelaiti hiyo unatarajiwa kutoa usaidizi katika kukusanya taarifa zitakazosaidia katika kilimo na usalama, kutabiri hali ya hewa na hata kukabiliana na majanga.

Wahandisi kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi wakisaidiwa na maafisa kutoka shirika la anga za juu la Japan walitengeneza chombo hicho katika mradi uliogharimu zaidi ya dola milioni moja.

Satelaiti hiyo itatumika kuchunguza mienendo ya kilimo, pamoja na kuchunguza maeneo ya pwani ya taifa hilo.

Wahadhiri wa vyuo vikuu wanasema satelaiti hiyo inaweza kutoa huduma tofuati ikiwemo kukusanya taarifa zitakazosaidia katika kilimo na usalama, kutabiri hali ya hewa na hata kukabiliana na majanga.

Kenya kwa sasa inakabiliwa na janga la mafuriko ambalo limesababisha maafa makubwa.

Japan ilitoa ufadhili na jukwaa la kuitengenezea lakini Wakenya wenyewe ndio waliitengeneza.

Satelaiti hiyo itatumwa hadi Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) na kuanza kuizunguka dunia kwa mwezi mmoja baadae.

Hatua hii itaifanya Kenya kuwa miongoni mwa mataifa mengine saba barani Afrika yaliyo na satilaiti zinazoizunguka dunia.

Mataifa hayo ni Misri, Afrika Kusini, Morocco, Algeria, Nigeria, Mauritius na Ghana.

Kwa mujibu wa chanzo cha serikali, Kenya itaanza kushughulika kuunda satelaiti kubwa na bora zaidi iwapo uzinduzi wa leo utafanikiwa.

Uzinduzi wa satelaiti hiyo leo unatokana na ushirikiano kati ya Idara ya Uhandisi katika Chuo Kikuu cha Nairobi, afisi ya masuala ya anga za juu ya Umoja wa Mataifa, na Shirika la utafiti wa anga za juu la Japan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.