Pata taarifa kuu
BURUNDI-HAKI

Mwanaharakati wa haki za binadamu ahukumiwa miaka 32 jela Burundi

Mahakama nchini Burundi imemuhukumu mwanaharati Germain Rukuki kifungo cha miaka 32 jela baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki katika maandamano dhidi ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza wakati akiwania muhula wa tatu.

Jengo la mahakama, Bujumbura Burundi.
Jengo la mahakama, Bujumbura Burundi. Photo AFP/Esdras Ndikumana
Matangazo ya kibiashara

Germain Rukuki anatuhumiwa kushiriki katika vuguvugu lililojaribu mapinduzi ya kijeshi na utekelezwaji wa mauaji ya askari polisi Mei 13 mwaka 2015, tarehe ambayo kundi la wanajeshi waliojaribu bila mafaanikio kumpindua rais Nkurunziza.

Mnamo mwezi Februari mwaka huu wanasheria wa Germain Rukuki, mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Burundi, waliomba kuahirishwa kwa kesi ya mteja wao inayosubiriwa na watu wengi nchini humo.

Alifungwa tangu Julai 13, 2017, akishutumiwa "kujaribu kuhatarisha usalama wa nchi " na "uasi" kwa kushirikiana na shirika la haki za binadamu la Acat-Burundi, ambalo lilipigwa marufuku nchini Burundi kama mashirika mengi ya haki za binadamu nchini humo.

Mwendesha mashitaka aliongeza makosa mapya katika kesi hiyo - mauaji, uharibifu wa mali ya umma, jaribio la kupindua utawala uliochaguliwa kidemokrasia, makosa ambayo upande wa utetezi haukuweza kufahamishwa. Hali hiyo ilipelekea wanasheria wa mwanaharakati huyo kuomba kesi inayomkabili mteja wao iahirishwe.

Kiongozi wa Acat-Burundi, Armel Niyongere, amesema anashangazwa na kesi ya mfanyakazi wake. Amebaini kwamba serikalini inaamini kwamba wanaharakati wa haki za binadamu waliosalia nchini wamekua wakitoa taarifa kwa wenzao walio uhamishoni.

Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International linabaini kwamba kesi inayomkabiliwa Bw Rukuki na ile inayowakabili wenzake wanne au wanaharakati wa zamani waliofuatiliwa katika kesi zingine inaonyesha utayari wa serikali ya Bujumbura kukandamiza anayethubutu kuikosoa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.