Pata taarifa kuu
UGANDA-RWANDA-DIPLOMASIA

Rais Museveni na Kagame kujadiliana kuhusu hali ya diplomasia kati yao

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake Paul Kagame wa Rwanda pembezoni mwa kikao cha Umoja wa Afrika wiki ijayo jijini Kigali, kujadili masuala tata yanaonekana kutikisa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Uganda Yoweri Musveni (Kushoto) akisalimiana na rais wa Rwanda Paul Kagame (Kulia) katika siku zilizopita
Rais wa Uganda Yoweri Musveni (Kushoto) akisalimiana na rais wa Rwanda Paul Kagame (Kulia) katika siku zilizopita PHOTO | PRESIDENCY
Matangazo ya kibiashara

Masuala ya usalama na uhamiaji yamesalia tata, kati ya nchi hizi jirani.

Serikali ya Rwanda hivi karibuni, imekuwa ikilalamika kuwa, Uganda inawakamata raia wake na kuwazuia na kudai kuwa ni wahalifu.

Kigali ilikasirishwa baada ya wanafunzi kutoka nchini mwake  kukamatwa jijini Kampala hivi karibuni.

Uganda nayo imekuwa ikilalamika kuwa, Rwanda imekuwa ikituma maafisa wake wa usalama kisiri kwa lengo la kuwalenga maadui wa serikali ya Kigali bila ya kuiarifu.

Wiki hii, Waziri wa Mambo ya nje wa Rwanda na msemaji wa serikali Louise Mushikiwabo, alisema nchi yake inasikitishwa na Wanyarwanda kuendelea kuteswa nchini Uganda lakini akaeleza kuwa ana matumaini kuwa viongozi hao watamaliza changamoto zinazoshuhudiwa.

Waangalizi wa mambo wanasema huenda hatua ya rais Museveni kumfuta kazi Inspekta Mkuu wa Polisi Kale Kayihura, ilikuwa njia mojawapo ya kujaribu kutatua tofauti kati ya nchi hizo mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.