Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA

Kura ya maoni kuhusu katiba: Warundi walazimishwa kujiandikisha

Zoezi la kuandika wapigakura kuelekea kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba linaendeshwa haraka na raia wanalaani jinsi zoezi hilo linavyoendeshwa kimabavu.

Kulingana na ripoti ya HRW , vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd Imbonerakure,  walishiriki katika mauaji ya kikatili mkoani Cibitoke kati ya Desemba 30 na Januari 3.
Kulingana na ripoti ya HRW , vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd Imbonerakure, walishiriki katika mauaji ya kikatili mkoani Cibitoke kati ya Desemba 30 na Januari 3. Desire Nimubona/IRIN/www.irinnews.org
Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura wanatakao andikwa katika zoezi hilo watakua na fursa ya kupiga kura katika kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba inayopangwa kufanyika mnamo mwezi Mei lakini pia Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Katika muda usiozidi wiki mbili uliotolewa kwa zoezi hilo, kuanzia tarehe 8 hadi 17 Februari , Tume ya Uchaguzi (Ceni) inasema imeridhishwa na idadi ya watu ambao wameshajiandikisha.

Tume hiyo inahakikisha kwamba hadi jana Alhamisi Februari 14 58% ya wapigakura waliotarajiwa walikuwa wamesajiliwa. Lakini upinzani, mashahidi na vyombo vya habari vya kujitegemea vinavyoendelea kurusha matangazo yao nchini Burundi vinashtumu kwamba araia wanalazimishwa kwa nguvu kujiandikisha, na tayari wameanza kufanyiwa vitisho.

Baadhi ya wanafunzi walio na umri ulio juu ya miaka 15 ambao wameongea na Idhaa ya Kiswahili ya RFI mjini Bujumbura wamebaini kwamba wanalazimishwa na viongozi wa shule kuingia shuleni na kadi waliopewa baada ya kujiandikisha, kwa yule ambaye atakua hakujiandikisha anachukuliwa adhabu.

Hata baadhi ya raia kutka mikoani wamebaini kwamba wanafanyiwa vitisho vya kuuawa na kulazimika kwenda kujiandikisha wakati zimesalia tu siku zisizozidi 2. Zoezi hilo litamalizika kesho Jumamosi Februari 17.

Waandishi wa habari na mashahidi wanashutumu visa vinavyoendelea nchini Burundi, ambapo Imbonerakure, vijana kutoka chama tawala ambao Umoja wa Mataifa unawataja kuwa "wanamgambo", wamekua wakifunga shule na masoko wakiwalazimisha watu wote walio na umri wa miaka 16 kwenda kujiandikisha ili kupiga kura.

Mashahidi wengine wametaja vitisho vinavyofanywa na viongozi tawala kwa kutowapa mbolea wakulima baada ya kulipa fedha kutoka mifukoni mwao au kutopewa matibabu ikiwa hawajasajiliwa.

"Kwa sasa ni vigumu raia kutembea katika mkoa wa Bubanza, magharibi mwa Burundi, bila kuwa na kadi inayoonyesha kuwa umejiandikisha. "Tangu jana Alhamisi asubuhi, watu wote wanaosafiri katika mkoa huo wanatakiwa kusimama kwenye vizuizi vilivyowekwa barabarani na Imbonerakure kwa ushirikiano na polisi," mashahidi wamebaini.

Upinzani unasema "zoezi hilo la kulazimishwa" linakiuka sheria za nchi. Lakini kwa upande wa utawala, wanabaini kwamba mtu anajiandikisha kwa hiari yake. Hata hivyo serikali imekiri kuwa kuna baadhi ya kasoro zinazojitokeza.

"Kwa kila kitu kinachotokea leo, Imbonerakure zinanyooshewa kidole cha lawama," amesema Makamu wa rais wa Burundi, Gaston Sindimwo. Sitaki kuwa msemaji wa kundi hili, lakini kuna watu ambao wanaweza kujifananisha au kutumia jina la Imbonerakure kwa kufanya mabaya. Lakini upande wa serikali, tunahimiza tu wananchi kujiandikisha. "

Hata hivyo Gaston Sindimwo ameonya kuwa wale ambao hawatajiandikisha leo hawataweza kupiga kura katika Uchaguzi mkuu wa 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.