Mazungumzo ya amani kuhusu Sudani Kusini yaendelea Ethiopia
Mazungumzo mengine ya amani kuhusu Sudan Kusini yameanza tangu siku ya Jumatatu jijini Addis Ababa Ethiopia wakati huu jumuiya ya kimataifa ikionekana kukosa uvumilivu kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na pande zinazohasimiana kutoheshimu juhudi za wapatanishi.
Imechapishwa:
Mazungumzo haya ambayo yanasimamiwa na jumuiya ya kiuchumi na maendeleo IGAD ni muhimu kwa pande zinazozozana kuafikiana baada ya kushuhudia mazungumzo kama haya kutofua dafu kuzima machafuko nchini Sudan.
Wachambuzi wa mambo wanamtazamo gani kuhusu mazungumzo ya safari hii? Wakili Martin Oloo anazungumza nasi akiwa jijini Nairobi nchini Kenya.
IGAD na jumuiya ya kimataifa sasa imewaonya viongozi wanaohasimiana aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar na rais Salva Kiir ambapo toka watofautiane mwaka 2013 nchi hiyo imekuwa ikishuhidia vita.
Machafuko nchini Sudan Kusini yamegharimu maisha ya maelfu ya watu, huku wengine wakilazimika kuyahama makazi yao.