Pata taarifa kuu
RWANDA-JINAI-HAKI

Rwanda kupiga kura juu ya kanuni za makosa ya jinai

Wabunge nchini Rwanda wiki hii wataanza kupigia kura mswada mpya unaoeleza kanuni mpya za makosa ya jinai nchini humo.

Kigali, mji mkuu wa Rwanda, ambapo wabunge wanatazamia kupigia kura juu ya kanuni za makosa ya jinai.
Kigali, mji mkuu wa Rwanda, ambapo wabunge wanatazamia kupigia kura juu ya kanuni za makosa ya jinai. RFI/Stéphanie Aglietti
Matangazo ya kibiashara

Serikali, kupitia Tume ya Marekebisho ya Sheria ya Rwanda, ilianza kuchunguza kanuni mpya za makosa ya jinai za mwaka 2015 kama sehemu ya jitihada za kurejelea kuweka sawa mfumo sheria za makosa ya jinai nchini humo.

Serikali imekuwa ikibadilisha sheria hiyo tangu mwezi Oktoba mwaka huu.

Wizara ya Katiba na Sheria nchini humo inasema, lengo la mabadiliko hayo ni kufanya sheria hiyo kueleweka kwa urahisi na kukabiliana vilivyo na makosa mbalimbali.

Waziri wa Katiba ya SheriaEvode Uwizeyimana aliwaambia wabunge kwamba mabadiliko yaliyopendekezwa yanalenga kuifanya raihisi sheria ya makosa ya jinai katika kuitumia na nuifanya ngumu kwa kukomesha uhalifu, kuadhibu wale wote watakaopatikana na uhalifu huo na kukabiliana na wahalifu.

Katika mahojiano ya simu na gazeti la New Times jana Jumanne , Mbunge John Ruku-Rwabyoma alisema kama wabunge wenzake walikubaliana kuhusu ibara zote, Wanyarwanda watashuhudia mabadiliko mengi na watafurahi

Amebaini kwamba sheria kuhusu utoaji mimba, huenda ikakubaliwa na wabunge wenzake na, hii itakua ni hatua nzuri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.