Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Mkataba wa amani kuanza kutekelezwa Jumapili usiku

Mkataba wa kusitisha mapigano nchini Sudan Kusini kati ya wanajeshi wa serikali na waasi, unaanza kutekelezwa saa sita usiku siku ya Jumapili.

Waasi nchini Sudan Kusini, katika siki zilizopita katika makabiliano na wanajeshi wa serikali
Waasi nchini Sudan Kusini, katika siki zilizopita katika makabiliano na wanajeshi wa serikali REUTERS/Goran Tomasevic/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Hii ni kwa mujibu wa makubaliano yaliyotiwa saini wiki hii jijini Addis Ababa nchini Ethiopia wakati wa mazungumzo ya amani kati ya serikali na makundi ya waasi.

Lengo la mkataba huu ni kumaliza mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea kwa mwaka wa nne sasa, na kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na Mamilioni kuyakimbia makwao.

Mkataba huu unataka pande zote kuacha mara moja kupigana na kutojihusisha na vitendo ambavyo vinaweza kuleta vita.

Aidha, wanasiasa wote walioakamatwa pamoja na wanawake na watoto wanaozuiwa wanastahili kuachiwa huru mara moja.

Tayari kiongozi wa waasi na Makamu wa rais wa zamani Riek Machar amewaambia wapiganaji wake kuacha mapigano na kusalia kambini lakini wajilinde iwapo watashambuliwa.

Jumuiya ya Kimataifa imeonya kuwa wale watakaovunja mkataba huu, watachukuliwa hatua kali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.