Pata taarifa kuu
TANZANIA-SIASA

Rais Magufuli ataoa msamaha kwa wafungwa 8157 siku ya uhuru

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 8157 wakiwemo 61 waliohukumiwa adhabu ya kifo

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. 12 Juni, 2017
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. 12 Juni, 2017 Ikulu/Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika kwenye Uwanja wa jamhuri Mkoani Dodoma jana Jumamosi, Rais Magufuli amesema msamaha huo hautawahusu wafungwa waliohukumiwa kwa makosa ya jinai na waliohukumiwa kwa makosa ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Kusamehewa kwa wafungwa waliohukumiwa kunyongwa ni hatua ya kwanza kuchukuliwa katika historia ya taifa hilo katika awamu zote zilizopita za uongozi.

Hata hivyo idadi ya wafungwa wengine walioachiwa huru kutokana na makosa mbali mbali ni 1,821 ambao amesema kuwa wanapaswa kuachiwa mara baada ya tangazo lake huku wafungwa wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao.

Idadi hiyo ya msamaha kwa wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa katika awamu zote kuwahi kutokea na hasa zinazo wahusisha wafungwa wa kunyongwa na vifungo vya maisha

Msamaha uliotolewa pia umemhusu mwanamuziki wa zamani Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mtoto wake Johnson Nguza maarufu kama Papii Kocha ambao mwaka 2004 walihukumiwa kifungo cha maisha kwa kuwanyanyasa kingono watoto wa shule ya msingi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.