Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI-SIASA

Mgogoro wa kisiasa waendelea kuigawa Kenya

Nchini Kenya, madai ya zamani ya kujitenga kwa baadhi ya maeneo ya Kenya yameanza kuzungumziwa na baadhi ya viongozi wa taifa hilo, baada ya uchaguzi wenye utata wa Oktoba 26.

Mji wa Mombasa.
Mji wa Mombasa. © Victor Ochieng/Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Juma lililopita, Mkuu wa mkoa wa Mombasa, Hassan Joho, aliongoza mkutano kuhusu namna ya kupiga kura ya kujitenga kwa pwani ya Kenya, akielezea jinsi eneo hilo limekua likitengwa kihistoria. Ombi ambalo ililikataliwa na chama tawala pamoja na jumuiya ya kimataifa.

Hoja hiyo ilitolewa na Mkuu wa mkoa wa Mombasa, Hassan Joho, na ule wa Kilifi, Amason Kingi, pamoja na wawakilishi kumi na watano waliochaguliwa. Wanashutumu visa vya kuchukuliwa ardhi ya eneo hilo na Wakenya kutoka mikoa mingine, ukosefu wa uwakilishi katika serikali ya kitaifa na kutengwa kwa kiuchumi. Madai haya sio mapya. Pwani ya Kenya ina kundi linalodai uhuru wa eneo hilo, MRC, tangu mwaka 1999, ambalo kulingana na madai yake eneo hilo lilikua sehemu ya zamani ya pwani iliyokua chini ya milki ya uongozi wa Zanzibar.

Lakini mkutano wa siku Ijumaa ulionekana hasa kuongozwa dhidi ya serikali ya Uhuru Kenyatta. Wakuu wa mikoa ya pwani kutoa upande wa chama tawala hawakushiriki mkutano huo, na Najib Balala, Waziri kutoa eneo hilo, kwa upande wake, alilaani hotuba hatari. Mjadala huo umewashtua mabalozi wengi wa Ulaya, ambao walikwenda Mombasa mwishoni mwa juma lililopita kwa madhumuni ya "kuonyesha wazi kwamba Ulaya inafanya kazi na Kenya yenye umoja, na kwamba mradi hako sawa kiuchumi, “ chanzo cha kidiplomasia kimesema.

Mapema mwezi Agosti Mshauri wa kiuchumi wa Muungano wa upinzani NASA, David Ndii, aliibua mjadala mkali baada ya kusema katika mahojiano ya televisheni kuwa wakati umewadia kwa sehemu nyengine za Kenya kujitenga.

Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Githu Muigai, wakati huo, alikemea vikali maoni hayo akisema yataligawa taifa hata zaidi kwa misingi ya kikabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.