Pata taarifa kuu
TANZANIA-JAMII-HAKI

Polisi ya Tanzania yawatia nguvuni mashoga 12

Polisi nchini Tanzania, wamewakamata wanaume 12 wakiwemo raia wawili wa Afrika Kusini na mmoja kutoka nchini Uganda wanaotuhumiwa kuwa mashoga.

Polisi wa Tanzania wawaweka nguvuni mashoga 12 jijini Dar es Salaam
Polisi wa Tanzania wawaweka nguvuni mashoga 12 jijini Dar es Salaam DR
Matangazo ya kibiashara

Wanaume hao walikamatwa siku ya Jumatano jijini Dar es salaam, katika Operesheni ya kuwakamata mashoga nchini humo, baada ya watuhumiwa wengine kukamatwa mwezi uliopita visiwani Zanzibar.

Wanaume hao walikamatwa katika hoteli moja, walikokuwa wanakutaka na wanatarajiwa kupelekwa Mahakamani.

Mwezi Juni serikali ya Tanzania ilitishia kuwakamata wanaharakati wa haki za mashoga na kuahidi kuwafukuza wageni ambao wataunga mkono kutetea haki za mashoga.

"Napenda kuwakumbusha na kuonya mashirika yote na taasisi ambazo zinafanya kampeni na kudai kutetea maslahi ya mashoga (...) Tutawakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wote wanaohusika", alisema Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba katika hotuba aliotolea umma na kurushwa na gazeti la serikali la Daily News. "Kama kuna shirika katika nchi hii ambalo linasaidia na kutetea ushoga, basi shirika hilo litapoteza usajili wake hapa," aliongeza Bw Nchemba. Waziri alionya kwamba nchi yake bila kusita itamfukuza nchini raia yoyote wa kigeni anayedai kutetea haki za mashoga.

Mapema mwaka huu serikali ya Tanzania ilitishia kuchapisha orodha ya mashoga wanaouza miili yao kabla ya kuachana na mpango huo baadae.

Siku chache kabla, serikali ya Tanzania iliamuru kufungwa kwa vituo maalumu vya afya vinavyopambana dhidi ya Ukimwi, baada ya kutuhumiwa kuendeleza ushoga, uamuzi uliokosolewa vikali na Marekani.

Nchini Tanzania, tendo la ushoga linaadhabiwa kwa hukumu nzito gerezani, lakini hivi karibuni serikali ilipitisha sheria dhidi ya mashoga. Ushoga umepigwa marufuku katika nchi 38 kwa jumla ya 54 za Afrika na unaadhabiwa kwa hukumu ya kifo nchini Mauritania, Sudan na Somalia, kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.