Pata taarifa kuu
BURUNDI-AFYA

Burundi kukosa mamilioni ya dola kutoka Mfuko wa Kimataifa dhidi ya UKIMWI

Burundi imepoteza usimamizi wa pesa zilizotolewa na Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria kwa manufaa ya Programu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa.

Wagonjwa wa VVU wamekua wakikabiliwa na malaria mjini Bujumbura, Burundi.
Wagonjwa wa VVU wamekua wakikabiliwa na malaria mjini Bujumbura, Burundi. REUTERS/Darrin Zammit Lupi
Matangazo ya kibiashara

Mfuko huu wa Kimataifa umeingiza zaidi ya dola za Marekani milioni 275 nchini Burundi kwa miaka 14. Sababu ya uamuzi huu ni matumizi mabaya ya fedha hizi kama inavyoonekana katika barua ambayo Mfuko wa Kimataifa ilimtumiaWaziri wa Afya wa Burundi.

Kimsingi, taasisi inayohusika na kusimamia fedha hizo inakabiliwa na vikwazo kwa utendaji wake usiofaa. Mfuko wa Kimataifa unakumbusha katika barua yake kuwa alama yake haijawahi kupita B1, sawa na 2 kati ya 5, hasa kwa "kushindwa kwake katika nyanja ya urasimu wa fedha na utoaji wa zabuni".

Matokeo yake ni uwezo mdogo wa kutumia fedha. Kwa mfano, dola milioni 30, sawa na 35% ya misaada kwa Burundi, haitatumiwa mwishoni mwa mwaka huu, Mfuko wa Dunia umeonya. "Haishangazi," kwa mujibu wa viongozi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutoka nchi hiyo yanayohusika katika mapambano dhidi ya UKIMWI, ambayo yamemshtumu Waziri wa Afya.

Zoezi la kuajiri kinyume cha sheria, maamuzi ya kufukuza wafanyakazi kiholela, kuingiliwa kwa usimamizi kila kukicha, gharama za magari, baadhi ya watu walionya hadharani kwa miezi kadhaa kuwa ndio chanzo cha kuzorota kwa taasisi hii ya urasimu fedha hizo, shutma ambazo Waziri wa Afya wa Burundi Josiane Nijimbere amekanusha.

Akikabiliwa na vitisho vya vikwazo kutoka kwa Mfuko wa Dunia, Waziri Nijimbere alikuwa amependekeza kuwa usimamizi wa pesa zote ukabidhiwe ofisi yake. Mfuko wa Dunia umeamua kuwa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mpango wa chakula Duniani UNDP, kuchukua usimamizi wa zaidi ya dola milioni 72 ya misaada kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

"Hii ni adhabu kali kwa serikali ya Burundi, " mwanaharakati mmoja wa haki za binadamu nchini Burundi amesema. "Jambo zuri hapa ni kwamba wagonjwa wataendelea kunufika na fedha hizo," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.