Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Rais Kenyatta aishukia mahakama baada ya kufuta ushindi wake

Rais wa Kenya uhuru Kenyatta amekosoa uamuzi wa mahakama ya juu kufuta uchaguzi wa rais na kusema kuwa idara ya mahakama inashida na atairekebisha endapo atachaguliwa tena.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto Service de presse de la présidence kényane
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwa hisia mchanganyiko hapo jana mbele ya wabunge na maseneta wa chama cha Jubilee Ikulu jijini Nairobi rais Kenyatta amewashuruku wana Jubilee kwa utulivu nakuongeza kuwa wako tayari kwa uchaguzi wa marudio ingawa hawakubaliani na uamuzi huo.

Aidha rais Kenyatta ameitaka tume ya IEBC kutaja haraka tarehe ya uchaguzi na kuionya mahakama kutoingilia shughuli za tume hiyo na kuongeza kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya wafanyakazi wa tume ya uchaguzi na mipaka kama upinzani wanavyoomba.

Kwa upande mwingine rais Kenyatta amewaonya upinzani kuhusu kutafuta madaraka kwa mlango wa nyuma na kusema kwamba hilo haliwezekani isipokuwa kwa kushinda uchaguzi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.