Pata taarifa kuu
KENYA

Magavana nchini Kenya washtumiwa kwa kuwafuta kazi wafanyikazi wa serikali za Kaunti

Serikali Kuu nchini Kenya, inawashutumu baadhi ya Magavana waliochaguliwa kwa kuamua kuwafuta kazi wafanyikazi wa serikali za Kaunti kwa sababu hawakuwaunga mkono wakati wa kampeni.

Msemaji wa serikali ya Kenya Erick Kiraithe
Msemaji wa serikali ya Kenya Erick Kiraithe yutube
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali Erick Kiraithe amesema kuwa hatua hiyo haikubaliki kwa sababu wafanyikazi wa serikali za Kaunti waliajiriwa kwa mujibu kwa Katiba ya nchi hiyo.

Aidha, amesema ikiwa hali hii itaendelea basi huenda ikaleta mgawanyiko katika Kaunti mbalimbali nchini humo.

“Tunawaomba Magavana ambao wameamua kuwafuta kazi, wafanyikazi kutofanya hivyo, hili halikubaliki, linasikitisha,” amesema Kiraithe.

Gavana wa Machakos ambaye alifanikiwa kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili, aliwasimamisha kazi idadi kubwa ya wafanyikazi kwa madai ya ufisadi.

Hali kama hiyo imeshuhudiwa katika Kaunti ya Meru ambayo Gavana mpya Kiraitu Murungi, aliamua kuwatimua wafanyikazi wa serikali za Kaunti kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha.

Kuhusu mgomo wa Wauguzi unaendelea kwa miezi kadhaa sasa, serikali kuu imewaomba warejee kazini na kuwapa nafasi Magavana ambao ndio wameapishwa, kushughulikia madai yao.

Mgomo wa Wauguzi umewaacha wagonjwa wengi wakiendelea kuteseka, wakidai kutekeleza mkataba wa kuwaongezea mshahara.

Shughuli za kiafya nchini Kenya zinasimamiwa na serikali za Kaunti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.