Pata taarifa kuu
KENYA-USALAMA

Polisi wamuua mvamizi wa maakazi ya Naibu rais William Ruto

Polisi nchini Kenya wamesema wamempiga risasi na kumuua mtu aliyevamia makaazi ya Naibu rais William Ruto siku ya Jumamosi na kusabibisha kifo cha afisa mmoja wa Polisi.

Barabara ya kuelekea nyumbani kwa Naibu rais wa Kenya William Ruto, Magharibi mwa nchi hiyo.
Barabara ya kuelekea nyumbani kwa Naibu rais wa Kenya William Ruto, Magharibi mwa nchi hiyo. citizen tv
Matangazo ya kibiashara

Imeelezwa kuwa mtu huyo alikuwa amejihami kwa upanga, na alimduga askari aliyekuwa langoni na kumpokonya silaha yake, kabla ya kuingia katika makaazi ya Ruto ambaye kipindi hicho, hakuwa nyumbani.

Inspekta Mkuu wa Polisi Joseph Boinnet amesema hali sasa ni shwari katika makaazi ya Naibu Ruto ya Sugoi katika jimbo la Uasin Gishu, Magharibi mwa nchi hiyo, lakini uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Hata hivyo, kumekuwa na maswali mengi kuhusu namna tukio hilo lilivyotokea huku baadhi ya  wachambuzi wa mambo wakihoji uwezekano mvamizi huyo kufanikiwa kuingia katika makaazi hayo.

Polisi inasema, lengo la uvamizi huo bado halijafahamika.

Mbali na suala hili, siku nane kuelekea Uchaguzi Mkuu wanasiasa hasa wagombea urais wanaendelea na kampeni za lala salama.

Ushindani wa urais unasalia kuwa kati ya rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga mgombea wa upinzani kupitia muungano wa upinzani NASA.

Kenyatta kwa mara nyingine amekanusha madai kuwa jeshi linapanga kumsaidia kushinda Uchaguzi huo, madai ambayo Odinga ameendelea kusisitiza kuwepo kwa njama hizo.

Wakati uo huo, Polisi wanamtafuta Meneja wa idara ya Teknolojia Habari na Mawasiliano ICT katika Tume ya Uchaguzi, Christopher Musando. 

Ripoti zinasema kuwa Musando, alitoweka siku ya Ijumaa na haijafahamika yuko wapi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.