Pata taarifa kuu
BURUNDI-TANZANIA-EAC-USHIRIKIANO

Maswali yaibuka kuhusu ziara ya rais Nkurunziza nchini Tanzania

Wiki iliyopita, rais wa Burundi Pierre Nkurunziza alifanya ziara ya siri nchini Tanzania. Tangu mwaka 2015 baada ya jaribio la mapinduzi la Mei, ilikuwa ni mara ya kwanza rais Pierre Nkurunziza kufanya ziara nje ya nchi yake. Ziara ambayo ilikua muhimu, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Burundi.

(Picha ya zamani) Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, Bujumbura, Mei 16, 2016.
(Picha ya zamani) Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, Bujumbura, Mei 16, 2016. REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Burundi inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa tangu mwaka 2015, ambao ulitokana na rais Nkurunzizakuwania muhula wa tatu, ambao aliupata baada ya uchaguzi alioshinda. Mpaka sasa mazungumzo ya kuiondoa nchi ya Burundi katika mgogoro unaoendelea chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, yameshindikana. Serikali ya Bujumbura inakataa katu katu kuketi kwenye meza ya mazungumzo na upinzani ulio uhamishoni licha ya shinikizo kutoka jumuiya ya kimataifa na vikwazo vya Umoja wa Ulaya.

Vyanzo vya kidiplomasia vinaeleza kwamba kama Pierre Nkurunziza alikua akikataa kusafiri nje ya nchi mpaka sasa, ilikua kutokana na kuogopa kupinduliwa madarakani. Rais Pierre Nkurunziza hajashiriki katika vikao vingi vyaJumuiya ya Afrika Mashariki vilivyofanyika tangu wakati huo, wakati ambapo Burundi ilikua kila mara kwenye ajenda ya mazungumzo ya vikao hivyo. Mwezeshaji mkuu wa mgogoro wa kisiasa wa Burundi, rais wa Uganda Yoweri Museveni amejaribu angalau mara tatu kukutana na Rais Pierre Nkurunziza, bila mafanikio. Kila wakati, rais wa Burundi alitoa pingamizi ili kuepika kukutana na rais Yoweri Kaguta Museveni

Hata hivyo wakuu wa nchi kutoka ukanda wa afrika mashariki, hatimaye waliamua kumuagiza rais wa Tanzania John Magufuli kujaribu kumshawishi kushiriki katika mazungumzo ya amani. Ndio lengo la mkutano huo uliyofanyika wiki iliyopita katika mji wa Ngara, kilomita thelathini kutoka mpaka wa nchi hizi mbili. Pierre Nkurunziza alikubaliana kukutana na mwenzake wa Tanzania hasa kwa sababu Tanzania ina hoja zinazohitajika ili iweze kusikika. Kwanza, Burundi ni nchi inategemea Tanzania kwa kuingiza bidhaa zake kutoka nje. Serikali ya Bujumbura haingekataa mwaliko huo kwa kuogopa kumchukiza jirani yake mkuu.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia rais Pierre Nkurunziza alishinikizwa kushiriki mazungumzo bila masharti.

Burundi imeendelea kukumbwa na mgogoro wa kisiasa , wakati ambapo watu zaidi ya 1000 wamepoteza maisha kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu na zaidi ya watu 300,000 wamelazimika kuikimbia nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.