Pata taarifa kuu
UGANDA-MAHAKAMA

Viongozi wa Mashtaka wakwamisha kesi katika Mahakama za Uganda

Viongozi wa Mashtaka nchini Uganda wanakutana leo kuamua ikiwa wasitishe mgomo ambao umekuwa ukiendelea kwa karibu wiki moja sasa na kukwamisha kesi Mahakamani wakidai nyongeza ya mshahara.

Mahakama iliyo tupu jijini Kampala nchini Uganda
Mahakama iliyo tupu jijini Kampala nchini Uganda www.dw.com
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya serikali kuwaomba miezi mitatu kushughulikia madai yao na kuwaomba kurejea kazini ili kuepusha msongamano wa kesi mbalimbali nchini humo.

Majaji wamekuwa wakiashirisha kesi nchini Uganda kwa ukosefu wa viongozi hao wa Mashtaka.

Msemaji wa muungano wa Viongozi wa Mashtaka nchini humo Aliwali Kizito, ameiambia runinga ya NBS kuwa mkutano mkuu wa viongozi hao wa mashtaka ndio wanaoweza kusitsiha mgomo huo.

“Hatima ya mgomo wetu upo mikononi mwa Mkutano mkuu wa wanachama wetu, tutakutana leo na kuamua ikiwa tutakubali ombo la serikali kuusitisha mgomo huu au la,” amesema Kizito.

Mgomo huu umesababisha kucheleweshwa pia kwa kesi kuhusu mauaji ya aliyekuwa msemaji wa Polisi Andrew Felix Kaweesi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.