Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Wanasiasa nchini Kenya na Tume ya Uchaguzi washindwa kuelewana

Wagombea urais nchini Kenya wameshindwa kukubaliana na Tume ya uchaguzi nchini humo IEBC kuhusu kumaliza mvutano uliojitokeza wa kampuni ipi ipewe zabuni ya kuchapisha karatasi za nafasi ya urais kama ilivyoshauriwa na Mahakama kuu wiki iliyopita.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati IEBCKenya
Matangazo ya kibiashara

Wagombea hao ambao jana walikutana na viongozi wa Tume hiyo jijini Nairobi na kushindwa kukubaliana na mkutano wao na maofisa wa tume hiyo kumalizika bila ya kufikiwa kwa muafaka kuhusu kumaliza sintofahamu iliyojitokeza.

Muungano wa upinzani wa NASA ulifungua kesi kutaka kampuni ya Dubai iliyopewa zabuni ya kuchapisha karatasi za urais isitishe kwa kile muungano huo unasisitiza kanuni hazikufuatwa wakati wa utoaji wa zabuni yenyewe suala ambalo Mahakama Kuu ilikubaliana na upande wa upinzani.

Kwa saa kadhaa, wanasiasa hao walivutana kwenye chumba cha mkutano kila mmoja akimtuhumu mwenzake kwa kutaka kuhujumu uchaguzi wa Agosti 8, huku chama tawala cha Jubilee chenyewe kikitaka kutoshirikishwa kwenye mchakato huu.

Mwishoni mwa juma lililopita rais Uhuru Kenyatta alitoa matamshi yaliyoonekana ni kutishia muhimili wa mahakama ambapo alidai kuwa majaji wamekuwa wakipendelea upande wa upinzani na kwamba nia yao ni kutaka kuharibu uchaguzi wa mwaka huu.

Hata hivyo, Jaji Mkuu wa Kenya amemuonya rais Kenyatta dhidi ya matamshi aliyoyatoa na kumtaka asalie katika kufanya siasa na sio kuingilia uhuru wa mahakama.

Kuna wasiwasi kuwa huenda uchaguzi mkuu wa Kenya ukasogezwa mbele ikiwa pande zinazovutana hazitafikia makubaliano wakati huu tume ya uchaguzi IEBC ikiwa imewasilisha rufaa yake kupinga uamuzi wa awali.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.