Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI-SIASA

Tume ya uchaguzi Kenya kukutana na wagombea urais

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya, inakutana leo na wagombea urais kujadiliana kuhusu namna ya kupata zabuni mpya ya kuchapisha makaratasi ya kupigia kura ya urais.

Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wagombewakuu wawili katika uchaguzi wa urais nchini Kenya unaopangwa kufanyika mwezi Agosti.
Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wagombewakuu wawili katika uchaguzi wa urais nchini Kenya unaopangwa kufanyika mwezi Agosti. DR.
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unafanyika siku 29 kabla ya Uchaguzi Mkuu nchini humo, na unakuja baada ya Mahakama wiki iliyopita, kufuta zabuni iliyokuwa imetolewa hapo awali baada ya kubainika kuwa haikiuwa wazi na haikuwashirikisha wadau wote.

Wananchi wa taufa hilo nao wanatarajiwa kutoa maoni yao kuhusu zabuni ya uchapishaji wa karatasi hizo, kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo kabla ya IEBC kutoa tangazo jipya.

Hayo yakijiri rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameonya mahakama nchini humo akiitaka kutousaidia upinzani na kuhujumu uchaguzi unaokuja.

Uchaguzi wa urais utafanyika mwezi ujao ambapo uhuru Kenyatta anataka kuchaguliwa tena.

Ijumaa wiki iliyopita, mahakama kuu iliamrisha tume ya uchaguzi isichapishe makaratasi ya kupigia kura, baada ya upinzani kuwasilisha kesi mahakamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.