Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-EU

Waangalizi wa EU waonya uwezekano wa kutokea machafuko nchini Kenya

Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu nchini Kenya kutoka Umoja wa Ulaya wameonya uwezekano wa kutokea machafuko baada ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 8 mwezi ujao.

Waangalizi wa Umoja wa Ulaya Julai 3 2017 wakiwa jijini Nairobi
Waangalizi wa Umoja wa Ulaya Julai 3 2017 wakiwa jijini Nairobi www.theeastafrican.co.ke
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa waangalizi hao Marietje Schaake amesema wasiwasi huu umeendelea kutolewa na raia wa nchi hiyo, kipindi hiki cha kisiasa.

“Hakuna siri kuwa, kuna uwezekano wa kutokea kwa machafuko. Wakenya wana hofu. Idara ya usalama na ile ya Uchaguzi ina jukumu la kipekee kuhakikisha kuwa hili halitokei,” amesema Schaake.

Kauli za wanasiasa nchini Kenya zimekuwa zikizua hofu huku kila mmoja akivutia upande wake.

Siku ya Ijumaa, wagombea wakuu wa urais, Uhuru Kenyatta na Raila Odinga watakutana jijini Nairobi katika maombi ya pamoka kama ishara ya kuhimiza amani.

Viongozi wa dini nchini humo wamekuwa katika mstari wa mbele kuhimiza amani nchini humo.

Mwaka 2007, machafuko ya baada ya Uchaguzi yalisababisha vifo vya zaidi ya watu elfu moja na maelfu kuyakimbia makwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.