Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA

Besigye awataka Waganda kukataa marekebisho ya Katiba

Mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa mgombea urais nchini Uganda kupitia chama cha FDC Kizza Besigye, anawataka raia wa Uganda kuzuia majaribio ya kuirekebisha katiba ya nchi hiyo ili kuondoa kifungu cha katiba kinachoweka ukomo wa umri wa mtu kuwania urais nchini humo.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda  Kizza Besigye.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye. AFP PHOTO / ISAAC KASAMANI
Matangazo ya kibiashara

Besigye amesema mpango wa chama tawala NRM kuwa katika harakati hizo kuondoa kifungo hicho, kinachoweka ukomo wa mgombea urais kuwa na miaka 75, ni ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya nchi hiyo.

Mwanasiasa huyo ambaye amewania urais mara nne dhidi ya rais Yoweri Museveni bila mafanikio, amesema wananchi wa Uganda wana nafasi ya kuzuia majaribio hayo kwa njia ya amani.

Katiba ya Uganda inaeleza kuwa, mtu haruhusiwi kuwania urais akiwa na miaka 75, lakini pia inaeleza kuwa umri wa anayetaka kuwania urais ni lazima uwe 35 na kuendelea.

Vyombo vya Habari nchini humo vinaripoti kuwa, tayari mswada huo umechapishwa katika Gazeti la serikali.

Wabunge wa NRM wanaounga mkono marekebisho hayo, wanasema sheria hii ikiendelea kuwepo itaendelea kuwa kikwazo kwa raia wa nchi hiyo wenye umri mkubwa, walio na uwezo wa kuendelea kuongoza nchi hiyo.

Duru kutoka ndani ya chama cha NRM, zinasema tayari mikakati inapangwa kutafuta maoni ya wananchi katika Wilaya mbalimbali ili kuirekebisha.

Mpango umeonekana wazi kuwa unalenga kuendelea kumtengezea mazingira rais Yoweri Museveni kuwania tena urais mwaka 2021, atakapokuwa na umri wa miaka 76.

Rais Museveni ambaye amekuwa akisema tatizo la Uganda na Afrika sio la viongozi kukaa madarakani kwa muda mrefu, bali ni kitu gani wanachoweza kuwafanyia wananchi.

Kiongozi huyo ambaye kwa sasa ana miaka 72, ameonekana kutokuwa tayari kuondoka madarakani hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.