Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-UHURU

Salva Kiir: Hatujutii uhuru tulioupata

Siku ya Jumapili Julai 9, nchi ya Sudan Kusini iliadhimisha miaka 6 tangu ipate uhuru wake bila ya kuwa na sherehe zozote jijini Juba wakati huu taifa hilo pia likishuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wakati wa maadhimisho ya miaka 6 ya uhuru wa Sudan Kusini, Rais Salva Kiir Alihutubia taifa, Julai 9, katika ikulu ya rais mjini Juba.
Wakati wa maadhimisho ya miaka 6 ya uhuru wa Sudan Kusini, Rais Salva Kiir Alihutubia taifa, Julai 9, katika ikulu ya rais mjini Juba. REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Robo tatu ya raia wa nchi hiyo wamelazimika kukimbia makazi yao na kusababisha kushuhudiwa kwa janga kubwa la wakimbizi kuwahi kushuhudiwa kwenye taifa hilo.

Nhial Bol Aken, mwandishi wa habari aliyeko mjini Juba, nchini Sudan Kusini ameiambia idhaa ya Kiswahili ya RFI kuwa hali si ya kuridhisha na kwamba kwa zaidi ya miezi minne wafanyakazi hawajalipwa mishahara yao.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, katika hotuba alioitoa kwa siku hiyo, alisema raia wake hawajutii uamuzi wao wa kupiga kura ya kutaka uhuru wao, licha ya kuwepo mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hiyo changa.

“imefika wakati wa kujifunza kutokana na makosa ya zamani na kuungana kuijenga Sudan Kusini, “ Rais Salva Kiir alisema.

Machafuko nchini Sudan Kusini yamesababisha vifo vya maelfu ya watu, na mamilioni wamehama makazi yao, tangu machafuko hayo yalipoanza mwezi Desemba mwaka 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.