Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Sudani Kusini yafuta tena sherehe za uhuru wake

Sudan Kusini ,ambayo ni taifa dogo zaidi ulimwenguni lililojaa vita vya wenyewe kwa wenyewe, imefuta sherehe za uhuru wake kwa mwaka wa pili mfululizo.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir The Japan Times
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali Michael Makuei ameelezea sababu za kufutwa kwa sherehe hizo kuwa ni kutokana na hali inayowakumba ambapo watu wanahitaji pesa hizo badala ya kuzitumia kwa sherehe.

Sudani kusini ilijintenga na Sudan mnamo Julai 9 mwaka 2011 lakini imetumbukia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013.

Mapigano na njaa vimesababisha vifo vya makumi kwa maelfu ya watu na kulazimisha wengine milioni 3.7 kukimbia makazi yao.

Uchumi wake unaotegemea mafuta uko hatarini kuporomoka huku mfumuko wa bei ukiongezeka hadi zaidi ya asilimia 800 mwaka huu.

Sherehe za mwaka jana pia zilifutwa kutokana na machafuko mjini Juba kati ya vikosi vya rais Salva Kiir na vikosi tiifu kwa makamu wa rais wa zamani Riek Machar.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.