Pata taarifa kuu
EAC-EU

Mahakama ya EAC yakataa ombi la Tanzania kuhusu EPA

Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Tanzania kupinga mkataba wa kibiashara kati ya Mataifa ya Jumuiya hiyo na Umoja wa Ulaya EPA.

Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki EACJ
Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo imekataa kusikiliza ombi la Tanzania kutaka mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutotia saini mkataba huo wa kibiashara.

Tanzania, Uganda na Burundi hazijatia saini mkataba huo kwa madai kuwa hauna maslahi ya mataifa hayo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo, tayari Kenya na Rwanda zimetia saini mkataba huo.

Jaji wa Mahakama hiyo Isaac Lenaola, pia hakuizuia Kenya na Rwanda kuendelea na mipango mingine kuhusu mkataba huu.

Uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hata hivyo umekubaliana kwenda nchini Ubelgiji kuzungumza na viongozi wa Umoja wa Ulaya kuhusu mkataba huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.