Pata taarifa kuu
KENYA

Polisi watatu wauawa nchini Kenya baada ya kukanyaga bomu lililotegwa ardhini

Maafisa watatu wa Polisi wameuawa katika eneo la Liboi katika Kaunti ya Garissa Kaskazini mwa nchi ya Kenya, baada ya gari walimokuwa wanasafiria kukanyaga bomu lililokuwa limetegwa ardhini.

Gari la Polisi nchini Kenya lililoharibiwa na bomu lililotegwa ardhini
Gari la Polisi nchini Kenya lililoharibiwa na bomu lililotegwa ardhini irinnews.org
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema maafisa wengine wawili walijeruhiwa katika shambulizi hilo.

Polisi hao walikuwa katika ziara yao ya kila siku katika mpaka wa Somalia, eneo ambalo linaaminiwa kuwa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al Shabab.

“Gari la Polisi lilikanyaga bomu lililotegwa ardhini. Wale wote waliopoteza maisha wametokea katika kituo kimoja cha Polisi,” amesema Kamishena wa eneo la Kaskazini Mashariki Mohammud Ali Saleh.

Maafisa wa usalama nchini Kenya wamekuwa wakiripoti  matukio ya magaidi wa Al Shababa kuingia nchini humo na kutenga mabomu ardhini kwa lengo la kushambulia maafisa wa usalama wanaowasaka.

Inspekta Mkuu wa Polisi nchini humo Joseph Boinnet amesema maafisa wake wanfanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa nchi hiyo inasalia salama.

Al Shabab wamekuwa wakilenga kuishambulia Kenya tangu mwaka 2011, ilipowapeleka wanajeshi wake nchini Somalia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.