Pata taarifa kuu
MAREKANI-SOMALIA

Marekani kusaidia jeshi la Somalia kupambana na Al Shabab

Marekani itapeleka wanajeshi wake wachache nchini Somalia kusaidia jeshi la taifa na kufanya operesheni za kiuslama ambazo bado hazijajulikana, msemaji wa jeshi la Marekani amesema jana Jumamosi.

Askari wa Somalia katika eneo la shambulizi mjini Mogadishu, Januari 2, 2017.
Askari wa Somalia katika eneo la shambulizi mjini Mogadishu, Januari 2, 2017. AFP
Matangazo ya kibiashara

Askari kutoka kitengo cha 101 cha anga, kikosi chepesi cha ardhini chenye mafunzo ya mashambulizi ya anga, kitatoa mafunzo na vifaa kwa jeshi la Somalia ili liweze kupambana na "kundi la Al Shabab msemaji wa Komandi ya Marekani Afrika iliyopo Ujerumani, Samantha Reho, ameiambia AFP.

Hapo jana nchi ya Ethiopia imeondoa majeshi yake katika mji muhimu katikati mwa Somalia, katika msururu wa hatua za hivi karibuni za taifa hilo kujiondoa nchini humo hatua ambayo inazorotesha mapambano dhidi ya kundi hilo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.