Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Upinzani nchini Sudan Kusini waanza mikakati ya kumwondoa madarakani rais Kiir

Viongozi wa vyama saba vya upinzani nchini Sudan Kusini wamekubaliana kuunda muungano wa kumwondoa rais Salva Kiir madarakani.

Kiongozi wa upinzani wa chama cha SPLM-IO Riek Machar
Kiongozi wa upinzani wa chama cha SPLM-IO Riek Machar nigeriatoday.ng
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni, viongozi hao walikuwa na mazugumo ya pamoja kwa njia ya simu na kukubaliana kuunganisha nguvu dhidi ya utawala wa Juba.

Aidha, wamekubaliana kukutana ana kwa ana hivi karibuni kuweka mikakati yao pamoja kuhakikisha kuwa umoja wao unakuwa na nguvu zaidi.

Wanasiasa hao wanamshutumu rais Kiir kwa uongozi mbaya na kuendeleza mateso kwa maelfu ya raia wa nchi hiyo ambao wanauawa kwa sababu ya njaa na vita huku wengine wakiyakimbia makwao.

Muungano huo unaungwa mkono na chama cha SPLM-IO kinachoongozwa na Riek Machar, kiongozi wa chama cha FDP Gabriel Changson Chan, Thomas Tut Doap kutoka chama cha UDRA.

Wengine ni pamoja na Kosti Manibe kutoka chama cha SPLM-FD, kiongozi wa chama cha SSNMC Joseph Bakasoro, Lam Akol anayeongoza chama cha NDM na Thomas Cirillo Swaka, kiongozi wa chama cha NAS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.