Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Rais Kiir amfuta kazi Mkuu wake wa Majeshi Paul Malong

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametangaza kumfuta kazi mkuu wake wa majeshi na mtu wake wa karibu Paul Malong, imesema taarifa ya ikulu ya Juba.

Paul Malong aliyekuwa Mkuu wa majeshi nchini Sudan Kusini
Paul Malong aliyekuwa Mkuu wa majeshi nchini Sudan Kusini idtimes
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Paul Malong aliyekuwa akitajwa kama kinara wa ukabila kutoka kwenye kabila la rais Kiir la Dinka, nafasi yake imechukuliwa na Jenerali James Ajongo Mawut.

Msemaji wa rais Kiir, Ateny Wek Ateny amesema kuwa hatua hii ni katika muendelezo wa mabadiliko ambayo yanafanywa na rais Kiiri na kwamba nafasi ya ukuu wa majeshi inaweza kukaliwa na mtu kwa muda wa miaka 2 hadi minne na Malong ameshika nafasi hiyo kwa muda wa miaka 3.

Mwezi Februari mwaka huu maofisa kadhaa wa juu wa jeshi walitangaza kujiuzulu nafasi zao wakimtuhumu Malong kwa kuendesha vita ya ukabila dhidi ya makabila mengine.

Miongoni mwa walioondoka jeshini ni pamoja na luteni Jenerali Thomas Cirillo aliyetangaza kuunda kundi lake la uasi.

Malong anaelezwa kuwa ndiye aliyekuwa mpangaji mkuu wa mapigano yaliyotokea mjini Juba mwezi Julai mwaka jana na kusababisha kuvunjika kwa Serikali ya kitaifa kati ya rais Kiir na mpinzani wake Riek Machar.

Hatua hii inakuja wakati huu kukiwa na wasiwasi wa kuendelea kwa vita nchini humo kati ya waasi na wanajeshi wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.