Pata taarifa kuu
UN-SUDAN KUSINI-USALAMA

UN: Vikosi vya Sudan Kusini vyashambulia mji wa Kodok

Umoja wa Mataifa unasema jeshi la Sudan Kusini limeshambulia mji wa Kodok katika jimbo la Upper Nile na kusababisha wakaazi wa eneo hilo kukimbilia nchi jirani ya Sudan.

Wakaazi wa mji wa Kodok katika mji wa Upper Nile State, Sudan Kusini, waendelea kuyahama makaazi yao kufuatia mapigano yanayoendelea., on the border with Sudan, 1 August, 2012
Wakaazi wa mji wa Kodok katika mji wa Upper Nile State, Sudan Kusini, waendelea kuyahama makaazi yao kufuatia mapigano yanayoendelea., on the border with Sudan, 1 August, 2012 Reuters/Margaret Aguirre/International Medical Corps/Handout
Matangazo ya kibiashara

Inakadiriwa kuwa watu zaidi ya 50,000 wamekimbia makwao baada ya mapigano ya hivi karibuni yanayoelezwa kuwa kati ya jeshi la serikali na waasi.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishinikiza serikali ya Juba kuwarejesha wanajeshi kwenye kambi zao na kutekeleza mkataba wa amani.

Umoja wa Mataifa waitishia kuichukulia vikwazo vipya Sudan Kusini

Mapema wiki hii Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliitishia Sudan Kusini kuichukulia vikwazo vipya kama usitishwaji mapigano hautoheshimishwa. Baadhi ya wanadiplomasia walmeonya kutokea kwa mauaji ya kimbari nchini humo.

Itafahamika kwamba machafuko nchini Sudan Kusini yamesababisha maelfu ya watu kuuawa na wengine kulazimika kuyahama makaazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.