Pata taarifa kuu
RWANDA-VATICAN-UHUSIANO

Rais Paul Kagame ziarani Vatican

Rais wa Rwanda Paul Kagame amewasili Jumapili hii jioni katika mji wa Roma kwa ajili ya mkutano wa Jumatatu na Papa Francis. Ofisi ya rais wa Rwanda ndio imetangaza ziara hiyo kwenye akaunti yake ya Twitter.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame. DR
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu ni wa kipekee. Kwa miaka mingi serikali ya Kigali inalituhumu Kanisa Katoliki kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyotokea nchini Rwanda. Mwezi Novemba, serikali ya Rwanda iliidai Vatican kuomba radhi kwa niaba ya Kanisa Katoliki nchini Rwanda kwa kuhusika kwa baadhi ya wajumbe wake katika mauaji hayo.

Mkutano huo ulikuwa kwenye ajenda rasmi ya kiongozi wa Kanisa Katoliki, lakini ilithibitishwa na serikali ya Kigali katika siku ya Jumapili jioni. Kwa mujibu wa Ofisi ya rais wa Rwanda, Paul Kagame atafanyakatika mji wa Roma kwa mwaliko wa Papa Francis kwa majadiliano juu ya "mahusiano baina ya Rwanda na Vatican." serikali ya Rwanda haikutoa maelezo zaidi.

Tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari mwaka 1994, uhusiano kati ya serikali ya Kigali na Kanisa Katoliki bado yanadorora. Kanisa Katoliki inatuhumiwa hasa kwa ukaribu wake na utawala wenye msimamo mkali wa Kihutu wa wakati huo na kushiriki kwa viongozi wa kidini katika mauaji.

Ziara ya kwanza tangu kuwasili kwa Kagame madarakani

Mwezi Novemba mwaka jana, Kanisa Katoliki nchini Rwanda iliomba msamaha kwa niaba ya Wakristo wote waliohusika katika mauaji ya kimbari.

Msamaha kwa watu binafsi, si kwa Kanisa kama taasisi, alisema rais wa Tume ya Maaskofu nchini Rwanda.

wakati huo serikali ya Kigali ilisema kuwa msamaha huo hauna maanana ingelikua bora zaidi Vatican yenyewe iomba msamaha.

Je Paul Kagame amebadili msimamo wake juu ya suala hilo? Ziara ni kwa mara ya kwanza Rais Paula Kagame kukutana Papa tangu achaguliwe kama rais wa Rwanda mwaka 2000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.