Pata taarifa kuu
RWANDA-KISWAHILI-UTAMADUNI

Kiswahili kuanza kutumiwa kama lugha ya taifa nchini Rwanda

Bunge la Rwanda limepitisha mswada wa sheria wa kuidhinisha Kiswahili kuanza kutumiwa kama  lugha ya taifa. Wabunge wameitaka serikali kuweka mikakati ili raia wake waelewe lugha hii kwa haraka.

Wabunge wa Rwanda, Oktoba 29, 2015 jijini Kigali.
Wabunge wa Rwanda, Oktoba 29, 2015 jijini Kigali. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Muswada huo wa sheria uliopitishwa na wabunge wote walioudhuria bungeni ,ni badaa ya ufafanuzi uliotolewa na Waziri wa Utamaduni, na kuonyesha faida zitakazo patikana bada ya lugha hii kuongezeka  kwenye lugha 3 zinazokubalika nchini Rwanda ambazo ni Kifaransa, Kingereza, na Kinyarwabnda  .

Wabunge badaa ya kupokea mswada huo na kuupitisha, wameonyesha kupongeza serikali kuweka mbinu zitakazo saidia Wanyarwanda kuelewa lugha hii kwa haraka.

Iwapo sheria hii itaanza kutumika, Rwanda itaanza kufundisha Kiswahili shuleni na elimu ya watu wazima itaanza kutolewa ili raia wote wapate fursa ya kujifunza lugha hiyo.

Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na Rwanda kua mwanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, na kuwasaidia raia wake kutobaki nyuma kimaendeleo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.