Pata taarifa kuu
BURUNDI-NJAA-USALAMA

Zaidi ya familia 300 zatoroka makaazi yao kutokana na njaa mkoani Cibitoke

Watu zaidi ya 1792 kutoka vijiji vya Mparambo ya kwanza na ya pili, Rukana ya kwanza na I ya pili, Munyika ya kwanza na Gabiro wilayani Rugombo mkoani Cibitoke, kaskazini magharibi mwa Burundi wametoroka makaazi yao kufuatia ukame na uhaba wa chakula.

Njaa inayosababishwa na ukame katika mikoa ya Bubanza na Cibitike magharibi mwa Burundi, yapelekea raia wa baadhi ya vijiji kuyatoroka makaazi yao.
Njaa inayosababishwa na ukame katika mikoa ya Bubanza na Cibitike magharibi mwa Burundi, yapelekea raia wa baadhi ya vijiji kuyatoroka makaazi yao. Christophe Carmarans / RFI
Matangazo ya kibiashara

Wengi wao wamekimbilia katika vilaya jirani za Mugina na Mabayi mckoani Cibitoke, lakini pia kusini magharibi mwa Rwanda na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Raia hao wameondoka na baadhi ya mizigo yao, huku nyumba zikiwa zimefungwa. Mashamba ya mahindi, mihogo na maharage yameharibika kutokana na na jua kali. "Mvua za kwanza ambazo zingelianza kunyesha mwezi Septemba mwaka jana bado zinasubiriwa," mkaazi mmoja wa kijiji cha Mparambo ya kwanza. Kesi za wanafunzi kuacha shule zimeanza kujitokeza katika vijiji vingi vya wilaya ya Rugombo. Magonjwa yanayotokana na utapiamlo yameanza kwa watoto na watu wazima.

Katika mkoa jirani wa Bubanza baadhi ya raia wameanza kuuza mabati ya nyumba zao ili waweze kupata chakula.

Baadhi ya viongozi tawala wamesema kuwa wana hofu ya kuzuka kwa wizi na vitendo vingine viovu kutokana na njaa ambayo imeanza kubisha hodi katika mikoa hiyo.

Hivi karibu baadhi ya raia wa mikoa ya Kayanza na Kirundo walikimbilia nchini Rwanda kutokana na njaa ambayo imesababishwa na mashamba kuharibika kutokana na ukame.

"Tuna hofu ya kuongezeka kwa visa vya wizi na hali hiyo huenda ikasababisha watu kujichukulia sheria mkononi, ambapo mwezi akikamatwa anauawa. Hali hiyo huenda ikasababisha kutokea kwa mauaji makubwa, " Jacques Nibizi, mkuu wa kijiji cha Rukana ameonya. Kiongozi huyo amesema hivi karibu kuna mtu aliyeuawa akijaribu kuiba.

Kwa mujibu la gazeti la Iwacu, tayari viongozi tawala katika mkoa wa Cibitoke wameanzisha zoezi la kuwatambua raia wanaokabiliwa na uhaba wa chakula pamoja na waathirika wa majanga ya asili ili waweze kuwasaidia. "Watu wanaohitaji msaada wa chakula ni wengi na wengi ni kutoka wilaya za Buganda na Rugombo, " kimebaini chanzo cha serikali ambacho hakikutaka jina lake litajwehuku kikiongeza kuwa uhaba wa chakula unaweza kusababisha kulipuka kwa magonjwa kama vile malaria na kipindupindu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.