Pata taarifa kuu
UGANDA-ICC-LRA

ICC: kesi ya Dominic Ongwen, kiongozi wa zamani wa LRA kusikilizwa tena

Kesi ya Dominic Ongwen, mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa kundi la waasi la LRA, itasikilizwa tena Jumatatu hii Januari 16 mjini Hague. Dominic Ongwen atajibu mashtaka 70 yanayomkabili mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Mauaji, ubakaji, mateso, utekaji nyara kwa watotoni miongoni mwa mashtaka yanayomkabili.

Mkuu wa zamani wa LRA, Dominic Ongwen,wakati akisikilizwa mbele ya mahkama ya ICC tarehe 6 Desemba 2016 mjini Hague.
Mkuu wa zamani wa LRA, Dominic Ongwen,wakati akisikilizwa mbele ya mahkama ya ICC tarehe 6 Desemba 2016 mjini Hague. REUTERS/Peter Dejong/Pool
Matangazo ya kibiashara

Kesi hii inasubiriwa na maelfu ya waathirika kwa sababu ni ya kwanza kushughulikia uhalifu uliofanywa na LRA kwa karibu miaka 30.

Baada ya kesi hii kufunguliwa mwezi Desemba, mashahidi wa kwanza wataanza kusikilizwa leo Jumatatu.

Mtu wa kwanza ambaye atasikilizwa, ni mtaalam wa kundi la Lords Resistance Army (LRA). Mtaalamu wa kaskazini mwa Uganda, kutoka jamii ya Acholi na LRA, shahidi huyo anatazamiwa kutoa ufafanuzi muhimu kuhusu kundi hili la wanamgambo wenye itikadi za mauaji.

Kwa upande wa mashtaka wako tayari kuonyesha kuwa kundi hili la waasi liliandaliwa kijeshi, ikiwa ni pamoja na vitengo vinne ambavyo viko chini ya amri ya Joseph Kony. pia kuonyesha kwamba Dominic Ongwen alikuwa na nguvu halisi wakati alipokuwa mmoja wa viongozi watano wa LRA katika uongozi wake binafsi wa kikosi cha wapiganaji 300 na jinsi gani maamuzi yake na ufanisi wake ulichangia kulipa nguvu kundi hili kati ya mwaka 2002 na 2005.

Katika kikao hiki cha kwanza, upande wa mashtaka utajikita kwenye mawasiliano ya redio iliyotekwa na jeshi la Uganda ambapo Dominic Ongwen alisikika akitoa amri. Changamoto bila shaka ni kuonyesha kwamba Dominic Ongwen mwenyewe aliamuru na kutekeleza mauaji, uporaji na ubakaji wakati wa mashambulizi manne katika makambi ya wakimbizi wa ndani ambayo anatuhumiwa kati ya mwezi Julai 2002 na mwezi Desemba 2005.

Na kuonyesha kwamba alijua anachokifanya kuwa ulikua uhalifu, kinyume na kile wanasheia wake wanachosema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.