Pata taarifa kuu
UGANDA-ICC-ONGWEN

Kiongozi wa zamani wa LRA akana mashataka dhidi yake

Aliyekuwa kamanda wa juu katika kundi la waasi wa Uganda wa Lord's Resistance Army, LRA, Dominic Ongwen, Jumanne hii Desemba 6, amekana mashtaka yanayomkabili baada ya kusomewa mashtaka 70 ya makosa ya kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, mbele ya majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, iliyoko The Hague, Uholanzi.

Mkuu wa zamani wa LRA, Dominic Ongwen, akisikilizwa katika kesi yake tarehe 6 Desemba 2016 mjini Hague.
Mkuu wa zamani wa LRA, Dominic Ongwen, akisikilizwa katika kesi yake tarehe 6 Desemba 2016 mjini Hague. REUTERS/Peter Dejong/Pool
Matangazo ya kibiashara

Awali wakati akifungua kikao cha mahakama kwaajili ya kusoma mashtaka yanayomkabili Ongwen, jaji kiongozi kwenye kesi hii, Bertram Schmitt, ametupilia mbali mapingamizi yote yaliyowasilishwa na upande wa utetezi waliotaka mteja wao kupimwa akili kwanza ili kujua ikiwa ana stahili kusimama kizimbani au la.

Jaji Schmitt katika uamuzi wake kupitia majaji wengine wawili wanaosikiliza kesi hiyo, ameeleza kusikitishwa na upande wa utetezi kuamua kuibua masuala ambayo yangeweza kuwa yameibuliwa wakati wa mchakato wa ufunguzi wa kesi yenyewe.

"Napenda niseme wazi kuwa, mahakama hii haitavumilia kuona upande wa utetezi unatumia mbinu zisizo za kitaalamu, kutaka kuchelewesha shauri hili kwa makusudi," alisema jaji Schmitt.

"Baada ya kupitia mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa utetezi, moja wakitaka mteja wao kupimwa afya ya akili na pia ushahidi kutafsiriwa katika lugha ya Chol, mahakama hii haijaridhishwa na hoja za upande wa utetezi na hivyo inatupilia mbali hoja hizo," alimaliza jaji Schmitt.

Baada ya kutoa maelezo ya utangulizi, majaji wa mahakama hiyo waliagiza kusomwa kwa mashtaka yote sabini na karani wa mahakama.

Mashtaka aliyosomewa Ongwen, yanahusu makosa ya kivita, uhalifu dhidi ya binadamu hasa kuhusu vitendo vya ubakaji, mauaji ya kiholela, kulazimisha watu kuhama makazi yao, utumikishaji wa watoto katika jeshi, udhalilishaji wa kingono na utumwa.

Akiulizwa ikiwa anafahamu na kuelewa mashtaka yaliyoko mbele yake, Ongwen alijibu "nakumbuka kuulizwa kuhusu hili swali, lakini napenda nisisitize kuwa, mashtaka haya ni dhidi ya kundi la LRA na mimi sio LRA, LRA ni Joseph Kony," aliwaambia majaji Dominic Ongwen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.