Pata taarifa kuu
ICC-UGANDA-ONGWEN-SHERIA

ICC yathibitisha mashitaka 70 dhidi ya Dominic Ongwen

Jumatano hii, Machi 23, majaji wa uhalifu wa kivita wamethibitisha mashitaka 70 dhidi ya mkuu wa zamani wa kundi la waasi wa Uganda (LRA) Dominic Ongwen kwa uhalifu uliofanywa nchini Uganda, ikiwa ni pamoja na kuwafanya watu watumwa wa ngono na kuajiri askari watoto.

Dominic Ongwen, kiongozi wa zamani wa kundi la waasi wa Uganda la LRA, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Hague, wakati ukisikilizwa uthibitisho wa mashitaka dhidi yake, Januari 21, 2016.
Dominic Ongwen, kiongozi wa zamani wa kundi la waasi wa Uganda la LRA, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Hague, wakati ukisikilizwa uthibitisho wa mashitaka dhidi yake, Januari 21, 2016. © REUTERS/Michael Kooren
Matangazo ya kibiashara

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa (ICC) "wamethibitisha mashtaka 70 yalioletwa na mwendesha mashitaka dhidi Dominic Ongwen," Mahakama kimataifa ya Hague imesema, huku ikibaini kwamba "imeanza kushughulikia kesi ya madai ya uhalifu wa kivita dhidi ya mtuhumiwa huyo."

Dominic Ongwen ambaye anajulikana kwa jina la "White Ant" katika lugha yake ya asili ya Acholi, anakabiliwa na mashitaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa kuhusika kwake mwaka 2002 na 2005 baada ya kujiunga na kundi hilo la kigaidi la waasi kaskazini mwa Uganda,likiongozwa na Joseph Kony anayesakwa na Marekani.

Ongwen atakuwa afisa wa kwanza wa kundi la waasi la LRA kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC), iliyoanzisha mwaka 2002 ili kukabiliana na uhalifu mkubwa ambao ulikua umekithiri ulimwenguni.

Ongwen ambaye alitekwa na kuingizwa katika kundi la waasi la LRA bado akiwa mtoto, alikuwa wakati mmoja naibu wa Joseph Kony na mmoja wa maafisa waandamizi wa LRA. Dominic Ongwen anatuhumiwa kuwaua watu zaidi ya 100,000 na kuwateka watoto 60,000 katika mashambulizi dhidi ya mji wa Kampala mwaka 1986.

Waendesha mashitaka mwezi Januari waliwaambia majaji wa ICC kwamba Ongwen alikuwa "mtu hatari" wa kundi ambalo liliendesha vitendo viovo katika nchi kadhaa za Afrika mashariki na kati.

Ongwen, mwenye umri wa miaka 40, inadaiwa kuwa aliamuru mauaji ya raia kama vile utekaji nyara na utumwa kwa kuwalazimisha watoto kuwa askari wa waasi, wakati kundi la LRA lilipokua likishambulia vijiji na maeneo ya mashambani, waendesha mashitaka wamesema.

Mashahidi wa mauaji walisema Ongwen aliamuru mateka wake, angalau katika tukio moja, "kuua, kupika na kula nyama za watu," waendesha mashitaka wameongeza.

LRA kwanza iliibuka kaskazini mwa Uganda mwaka 1986, ambapo ilidai kupigana kwa jina la kabila la Waacholi dhidi ya serikali ya Uganda iliyokua ikiongozwa na Rais Yoweri Museveni.

Lakini kadri miaka inavyokwenda kundi la LRA, liliendelea na maovu yake nchini Uganda likihama hama, hadi kuvuka mipaka na kuingia katika nchi jirani, kama vile, Sudan Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Machi 2008.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.