Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-USALAMA

Watu 21 wauawa katika shambulizi kusini mwa Sudan Kusini

Watu ishirini na moja, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, waliuawa Jumamosi katika shambulizi lililohusishwa waasi wa Sudan Kusini kwenye barabara inayotokea mji mkuu, Juba, katika mji wa Yei, kusini mwa Sudan Kusini inayokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwishoni mwa mwaka 2013, polisi imetangaza Jumatatu hii.

Mkimbizi akiandamana na askari wa kulinda amani, karibu na kambi ya kulinda raia (POC) ya Umoja wa Mataifa mjini Juba, Oktoba 4, 2016.
Mkimbizi akiandamana na askari wa kulinda amani, karibu na kambi ya kulinda raia (POC) ya Umoja wa Mataifa mjini Juba, Oktoba 4, 2016. ALBERT GONZALEZ FARRAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Lori lililokua likisafirisha raia walioyakimbia makazi yao kufuatia mapigano yanayoendelea kurindima kaskazini mwa nchi na walikua wakihamishwa katika wa Yei (kilomita 150 kusini magharibi mwa mji wa Juba) 'lilianguka mikononi mikononi mwa waasi,' Dominant Kawcgwok, Naibu msemaji wa polisi nchini Sudan Kusini ameliambia shirika la habari la AFP, na kuongeza kwamba wengi wa waathirika walikuwa wanawake na watoto.

'Tulipoteza watu 21' na ishirini walijeruhiwa, amesema Bw Kawcgwok.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Sudan Kusini, serikali ya Rais Salva Kiir imeonyooshea kidolea cha lawama katika shambulizi hili kwa waasi wanaomtii aliyekuwa Makamu wa rais na mpinzani wa Bw Kiir, Riek Machar.

Riek Machar alikimbilia katika mji wa Khartoum, nchini Sudan baada ya kukimbia mapigano yaliyosababisha vifo vya watu wengi mjini Juba mwezi Julai mwaka huu.

Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) umesema Jumatatu hii katika taarifa yake kwamba una 'taarifa inayotia wasiwasi kuhusu machafuko' dhidi ya raia katika mji wa Yei. UNMISS 'inatiwa wasiwasi mkubwa kuhusu kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama katika mji wa Yei (katika jimbo la Central Equatoria, ambapo ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini bado umeendelea kunyimwa haki ya kuingia eneo hilo.'

Katika tukio jingine, mabasi matatu ya abiria yanayofanya safari kati ya Juba na Uganda yameshambuliwa Jumatatu hii na watu wenye silaha wasiojulikana, ameongeza Bw Kawcgwok, alieleza kwamba hakuna abiria yeyote aliyejeruhiwa.

Akihojiwa na shirika la habari la AFP, msemaji wa polisi wa Uganda amethibitisha shambulizi hili la Jumatatu lakini amesema abiria kadhaa walitekwa nyara, bila hata hivyo kusema idadi halisi.

"Kulikuwa na shambulizi dhidi ya mabasi yaliyokuwa yakisafiri nchini Uganda, shambulizi lililotekelezwa na watu wenye silaha, upande wa Sudan Kusini (Jumatatu hii) asubuhi," Felix Kaweesa ameliambia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.