Pata taarifa kuu
EAC

Viongozi wa EAC, wataka nchi za magharibi kuacha kutoa tahadhari za kusafiri kwa raia wao

Viongozi kutoka ukanda wa nchi za Afrika Mashariki, wametoa wito kwa makampuni ya Kimarekanik kwenda kuwekeza kwenye nchik zao, wakitolea mfano maendeleo makubwa yaliyofanyika kwenye miundombinu yake.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni. REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, makamu wa rais wa Kenya, William Ruto na waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, wote kwa pamoja wameitaka Serikali ya Marekani kuacha mara moja tahadhari za kutosafiri kwa raia wake wanaopenda kusafiri kwenda kwenye nchik za ukanda.

Wakuu hao wa nchi wamewaambia wawekezaji wa Marekani kuwa, nchi 5 wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki, zimefanya uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu yake, ikiwemo reli, barabara, hoteli na kuboroshwa kwa safari za ndani ya nchi wanachama.

Viongo hao wamewahakikishia wawekezaji binafsi kutoka makampuni ya Marekani, kwenda kuwekeza kwenye ukanda huo, kwa kile walichosema kuwa, eneo lao ni miongoni mwa maeneo bora na salama zaidi kuwekeza.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni aliwaambia wawekezaji hao kuwa “eneo la Afrika Mashariki ni eneo bora kuwekeza. Ni eneo zuri kuwepo. Usalama ni mzuri. Lakini mnapaswa kuacha kutoa matangazo ya tahadhari ya kusafiri kwenye nchi hizo.” alisema Museveni.

Wakizungumza wakati wa mkutanok wao na waziri wa masuala ya biashara wa Marekani, Penny Pritzker, viongozi hao wametoa wito kwa Marekani kuhakikisha inaharakisha mchakato wa kuwa na ndege zake zinazofanya safari za moja kwa moja kwenye nchi hizo.

Viongozi hawa walieleza msimamo wao wa pamoja, wakati pia walipokutana na wakuu wengine wa dunia na watendaji wa makampuni mbalimbali ya dunia, ambapo waliwahahakikishia mazingira mazuri ya uwekezaji.

Wakuu hao wa nchi wamekiri kuwa matangazo ya tahadhari ya kusafiri kwenye nchi zao, yanaoendelea kutolewa na baadhi ya nchi za Ulaya, yameathiri uchumi wa mataifa yao na kuwaogopesha wawekezaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.