Pata taarifa kuu
KENYA

Wadau wa elimu nchini Kenya wakutana kwa dharura kujadili mabweni kuteketezwa moto

Wadau wa elimu nchini Kenya wanakutana kwa siku mbili jijini Nairobi kujadili mwendelezo wa visa vya wanafunzi wa shule za Sekondari za serikali kuendelea kuteketeza moto mabweni yao.

Moja ya bweni liliteketezwa moto
Moja ya bweni liliteketezwa moto West FM
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne, mabweni ya shule tano yalitekeletezwa moto hali ambayo imeendelea kuzua wasiwasi kuhusu hali ya nidhamu ya wanafunzi wa shule za sekondari nchini humo.

Mamia ya wanafunzi kutoka shule mbambali nchini humo wanazuiliwa baada ya shule 100 kuteketezwa moto mwaka huu.

Muungano wa kitaifa wa Walimu wakuu wa shule za sekondari wamekutana na Tume ya kuwaajiri walimu TSC kujadili namna ya kutatua tatizo hili.

Waziri wa Elimu Fred Matiang'i amelaani uteketezwaji huo kwa kile anachosema unachochewa na watu ambao hawataki mabadiliko katika sekta ya elimu nchini humo.

Miongoni mwa mabadiliko yaliyoletwa na Waziri huyo ni pamoja na kuongeza muda wa mihula shuleni na kupiga marufuku wanafunzi wa kidato cha nne, kutembelewa shuleni pamoja na kuwa na mikutano ya maombi muhula wa tatu wakati wanapojiandaa kufanya mtihani wao wa taifa.

Waziri huyo anasema anaamini mabadiliko hayo yatasaidia kupambana na udanganyifu wa mitihani ya kitaifa kama ilivyokuwa mwaka uliopita.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, ambaye yuko ziarani nchini Marekani amemshtumu Waziri wa Elimu kwa kulazimisha sera ambazo zimechangia  matukio haya.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.