Uganda kuondoa wanajeshi wake nchini Somalia mwaka ujao
Jeshi la Uganda linasema litaanza kuwaondoa wanajeshi wake wanaopambana na kundi la Al Shabab nchini Somalia mwaka ujao.
Imechapishwa:
Uganda ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutuma kikosi chake nchini humo mwaka 2007, chini ya mwavuli wa AMISOM kwa lengo la kuilinda serikali iliyokuwa inaungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa.
Mkuu wa jeshi hilo la UPDF, Jenerali Katumba Wamala hajasema sababu kuu ya wanajeshi wa nchi yake kuondoka Somalia, ila amesema tu wakati hufika na mtu hurudi nyumbani.
Kuelekea kurejea kwa jeshi hilo la Uganda, limeendelea kushirikiana na Burundi, Djibouti, Ethiopia na Kenya kupambana na wanamgambo hao.
Mwezi uliopita, msemaji wa jeshi Paddy Ankunda alinukuliwa akisema jeshi la nchi hiyo lipo kwenye harakati za kurudi nyumbani.